KONGAMANO LA WADAU WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA(NHIF)NA MFUKO WA AFYA YA JAMII(CHF)MJINI BUKOBA TAREHE 29-03-2012
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeandaa kongamano la wadau la siku moja kwa ajili ya Wadau wa Bima ya Afya.
Kongamano hili limefanyi Mjini hapa(Bukoba) katika ukumbi wa Kolping Hotel kuanzia saa 2:00 asubuhi.
Mgeni rasmi katika Kongamano la wadau wa Bima ya Afya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh. Kanal Massawe akitoa hotuba ya Ufunguzi wa kongamano hili.
Wadau wa Kongamano la mfuko wa Taifa wa Bima ya Afaya wakifatilia hotuba ya Ufunguzi ya Mgeni rasmi.
Wadau wakitafakali na kujadili mada iliowasilishwa katika siku ya Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoa wa Kagera. |
Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Afya ya Jamii(CHF) akiongea juu ya taarifa ya CHF ya Mkakati wa Afya bora kwa wote.
Makamu Meya wa Manispaa ya Bukoba Ndg Ngalinda.
Wadau wa Mfuko wa Afya ya jamii wametoa maombi maalum kwa Uongozi wa Mkoa/Wilaya kuwa suala la CHF liwe agenda ya kudumu katika vikao vya mkoa na Wilaya,Viongozi wa Mkoa na Wilaya wasaidie katika suala la Uhamasishaji pia kuakikisha fedha za CHF zinaelekezwa katika katika Ununuzi wa Dawa na kuzihamasisha Halmashauri zitenge fedha kwa ajili ya kulipa makundi maalum na kutafuta wafadhili.
Wadau wakisikiliza Maombi Maalum kutoka kwa Mjumbe wa Bodi
Bodi imeomba Waratibu wa CHF wanaoteuliwa na Halmashauri wawe ni wale wanaofanya kazi za maendeleo ya jamii kama maafisa maendeleo ya Jamii na kwa Halmashauri ambazo mratibu wa NHIF na CHF ni mmoja wateuliwe wawili ili kuongeza Ufanisi.
Ni Muda wa Mapumziko na kupata Chai.
Baada ya Mapumziko wadau waliendelea na Majadiliano na na kupitia Miongozo Mbalimbali.
Picha ya pamoja ya Viongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Viongozi wa Serikali picha ya pamoja na Wadau wa Mfuko wa Taifa ya Afaya(NHIF).