Bukobawadau

MKUU WA MKOA AKABIDHI MSAADA WA BAISKELI KWA WALEMAVU WAWILI – KAGERA

Mkuu wa Mkoa Akimkabidhi Bw. Simon (Mlemavu) Baiskeli Tayari kwa Kumsaidia kwenye Shughuli zake.
Walemavu Wakifurahia Baiskeli zao Mara Baada ya Kukabidhiwa.


Mkuu wa Mkoa wa Kagera alikabidhi msaada wa Baiskeli za magurudumu matatu kwa walemavu wawili Bw. Simon Rudovick kutoka Kamachumu Muleba na Bi Sikudhani Ibrahim kutoka Kashai Manispaa ya Bukoba.


Hafla hiyo fupi ya kukabidhi  baiskeli za walemavu ilifanyika  jana tarehe 21/11/2012 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera.  Aidha Mwenyekiti wa chama cha walemavu Kagera CHAWATA alimweleza Mkuu wa Mkoa kuwasaidia walemavu katika  kufufua na kufunguliwa tena chuo cha Walemavu Migara Izimbya.
Chuo hicho kilianzishwa mwaka 1998 kwa ajili ya watoto wenye ulemavu kujifunza ufundi pia na kuwahudumia watoto wasiokuwa walemavu. Chuo hicho kilianzishwa kwa msaada wa wafadhili toka Swiden ambapo walitoa vifaa na kusimamia ujenzi lakini baada ya wafadhili haokumaliza muda wao na kuondoka chuo hicho kilifungwa mwaka 2009.
Mkuu wa mkoa alihaidi kulishughulikia tatizo hilo na kumwagiza Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa Bw. Charles Mafwimbo kuhakikisha Halmashauri za Wilaya zote mkoa wa Kagera  zinatenga fungu la kuendeleza chuo hicho na mwakani  kianza  tena kutoa huduma kwa wananchi.
Aidha Mhe. Massawe ametoa mwito kwa Taasisi na mashirika pia na watu binafsi kuwa na moyo kama wa Kampuni ya KUGIS waliotoa baiskeli mbili za walemavu zenye thamani ya shilingi laki sita ili kutoa misaada kama hiyo kwa walemavu. Pia amewataka walemavu kujihimu kufanya kazi na kujipatia kipato na kuacha tabia ya kuombaomba ili kujikwamua kimaisha badala ya kutegemea kuomba kila kukicha
Next Post Previous Post
Bukobawadau