Bukobawadau

WALIO JIRANI NA MGODI WA NICKEL NGARA WASHAURIWA KUPIMA VVU KWA HIARI

 Wananchi wanaoishi katika kata zinazozunguka mradi wa uchimbaji madini ya Nickel wilayani Ngara mkoani Kagera  wameshauriwa kupima afya zao kwa hiari ili kujikinga na maambukizi mapya ya Virusi Vya UKIMWI
Kauli hiyo imetolewa jana na  baadhi ya watu wanaoishi na maabukizi ya VVU wilayani Ngara katika mwendelezo wa maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani ambapo wilayani  Ngara yamehitimishwa katika kata ya Bugarama
Mmoja wa watu hao Bw  Epimarck Felician amesema kuwa kila atakayekutwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi atafute matibabu na kutumia dawa za kupunguza ukali wa virusi hivyo   na jamii iachanane na unyanya paa dhidi yake
 Bw Felician ametoa rai kwa vituo vya kutolea huduma za afya kuwapatia dawa na ushauri nasaha wanaoishi na maambukizi ya virusi vya UKIMWI ili waweze kuishi kwa matumaini na kufanya kazi za maendeleo
Kwa upande wake Bi Suzan Didas ambaye ni mmoja wa walimishaji rika anayeishi na virusi vya ukimwi ametoa wito kwa wanawake kuendelea kupima afa kwa hiari na wanaweza kuendelea na kuzaa watoto endapo watakubaliana na weza wao
Naye mwaelimishaji rika mwingine wa kata ya Rulenge Bi Dionesia Mbanza ameishauri wanaoishi na maambukizi ya VVU kuhudhuria  vituo vya huduma na kupewa ushauri nasaha na  dawa za kuzuia magonjwa nyemelezi .


Hata hivyo diwani wa kata ya Bugarama Bw Adronis Bulindoli amesema kuwa baadhi ya i wanaoishi na maambukizi ya virus vya ukimwi wamekuwa wakikwepa kwenda katika vituo vya kutolea huduma hali ambayo huchangia  unyanyapaa.
“Jitahidi kuepuka kueneza maambukizi ya VVU kwa makusudi kwani kufanya hivyo ni kudhoofisha jitihada ya serikali za kutokomeza virusi hivyo” Alisema Bulindoli
Bw Adroniz Bulindoli ametoa rai hiyo kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo Bw Costantini Kanyasu katika mwendelezo wa kuadhimisha siku ya ukimwi duniani ambayo imehitimishwa katani Bugarama wilayani Ngara
Amesema kuwa baadhi ya wananchi wanaoishi na maambukizi ya virus vya ukimwi wamekuwa na tabia ya kueneza ugonjwa huo na kuacha kwenda katika vituo vya kutolea
huduma hali ambayo huchangia kuwepo unyanyapaa.
 Katika kupata nasaha hizo watu 172 walioko katika kata za Bukiriro na Bugarama wilayani Ngara mkoani kagera siku hiyo wamepima maambukizi ya virusi vya ukimwi katika kampeni inayofanywa na shirika la Twesa na Right to Play yaliyoko  wilayani Ngara
 Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rulenge wilayani Ngara Bi Hilda Kagaruki amesema kuwa kati ya watu hao 120 ni kutoka kata ya Bugarama 52 ni wa kata ya Bukiriro na katika idadi hiyo ni watu wawili ndio wamekutwa na  VVU

Bi Kagaruki amewasihi wananchi kuendelea kupima afya zao ikiwa ni pamoja na kuwapa moyo wa matumaini wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa kuwajali na kuwasaidia mahitaji muhimu  kuliko kuwatelekeza na kuwanyanyapaa
Hata hivyo mratibu wa a Right to Play wilayani Ngara Bw Joramu Wimo amesema mashirika yanashirikiana na Kabanga Nickel pamoja na Halmashauri ya wilaya ya Ngara katika  kata tano zinazozunguka  mradi wa kabanga nickel wilayani humo.
(Katika Picha Bi Hilda Kagaruki akiwa katika zoezi la Upimaji  wananchi VVU na anayehutubia mwenye Tshirt ya Right to Play ni Mratibu wa shirika hilo wilayani Ngara Joramu wimo) 
Shirika la Right to Playa kwa kushirikiana na Kabanga Nickel Twesa na Halmashauri ya wilaya ya Ngara linahamasisha wananchi walioko kata za Bugarama Bukiriro Rulenge Muganza na Murusagamba kupima kwa hiari maabukizi ya VVU na kuelimisha jinsi ya kuepuka unyanyapaa kwa wanaoishi na HIV katika kata hizo
 Mh. Diwani wa kata ya Bugarama Bw Adronis Bulindoli akiongea na wananchi.

Next Post Previous Post
Bukobawadau