Bukobawadau

MKUU WA MKOA WA KAGERA AZINDUA WIKI YA MAJI KWA KUTEMBELEA MIRADI YA MAJI MKOA MZIMA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa shilingi billion 8.2 kwa mkoa wa Kagera ili kuhakikisha wananchi wa mkoa huu wanapata maji safi na salaama na yenye uhakika katika maeneo yao hususani maeneo ya vijijini ifikapo 2015.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa mkoa akizindua wiki ya maji Mkoani Kagrera tarehe 17/03/2014 katika Manispaa ya Bukoba. Mhe. Massawe katika kuadhimisha wiki ya maji anatembelea na kukagua miradi ya Maji inayotekelezwa katika  Halmashauri za Wilaya zote za mkoa wa Kagera
Mhe. Massawe alizindua wiki ya Maji alitembelea na kukagua mradi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira unaofadhiliwa na serikali ya Ufaransa kupitia Shirika lake la Maendeleo la  (AfD) unaotekelezwa katika Manispaa ya Bukoba  kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania na Mamlaka ya Majisafi na Maji taka Bukoba.
 Mradi huo utakaogharimu  Shilingi billion 27,528,304,236 tayari umetekelezwa kwa asilimia 30 na bado unaendelea kujengwa na Kampuni ya kutoka India (Technofab-Gammorn-Toddy Joint Venture) na Msimamizi / Mshauri  (Consultant) ni Laymer GKW Consult kutoka Ujerumani.
Baada ya mradi huo kuwa umekamilika unatarajia kutoa hudum ya maji katika kata 4 za Buhembe, Kagondo, Kahororo na Nyanga ambazo zikuwa hazipati huduma ya maji na kukamilisha huduma hiyo katika kata 14 ambapo wananchi watapata  maji kwa asilimia 90 kutoka  asilimia 75 za awali.
Pamoja na Mradi huo Manispaa ya Bukoba pia itanufaika na Miradi mingine mitatu ambayoni : Mradi wa Ujenzi wa Mfumo wa Kutibu Maji taka eneo la Nyanga. Mradi wa Mfumo wa majitaka (Kwaajili  ya eneo la Kati la mji wa Bukoba) utakaogharimu EURO 226,675 na unafadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia LVEMP II
 Pia mradi wa tatu ni wa Maji katika miji mikuu ya Wilaya 6 (Biharamulo, Bunazi/ Kyaka, Chato, Kayanga/Omurushak , Muleba na Ngara) na mradi huo utagharimu kiasi cha USD 817,800 na unafadhiliwa na Benki ya Dunia ikishirikiana na Serikali ya Tanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera anaendele na ziara ya kukagua miradi ya maji wilayani ambapo katika Wilaya ya Missenyi alitembelea na kukagua ujenzi wa Mradiwa Majia katika kijiji cha Rukulungo wenye gharama ya shilingi milioni 347, na umejengwa kwa asilimia 70.
Wilaya ya Kyerwa Mhe. Massawe alikagua mradi wa Maji Rwabikagati uliokamilika kwa asilimia 80 na utagharimu zaidi shilingi milioni 880. Katika Wilaya ya Karagwe Mhe. Massawe alitembelea na kukagua mradi wa Maji Chanika uliokamilika kwa asilimia 70 na utagharimu shilingi milioni 734 ukikamilika.
Baada ya kutembelea na kukagua miradi hiyo ya maji Mkuu wa mkoa alitoa maagizo kwa  Wakandarasi wa miradi hiyo kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati ili lengo la serikali litimie kwa wananchi  kwa kupata huduma ya maji  safi na salaama ifikapo 2015.
Mhe. Massawe pia aliagiza baadhi ya Kamati za maji ambazo ziliundwa na hazitekelezi majukumu yake ipasavyo zivunjwe na kuundwa upya ili kuleta ufanisi katika kuhaklikisha miradi ya maji inafanya kazi na kutunzwa kama inavyotakiwa.
Aidha Mkuu wa Mkoa alitoa agizo kwa taasisi za Serikali kuhakikisha zinalipa madeni ya  ankara zao za maji  kwani Taasisi hizo ndizo zinaongoza kwa Madeni jambo ambalo linazifanya Mamlaka za Maji  kushindwa kujiendesha na kuimarisha huduma za maji kwa wananchi.
Angalizo, Mhe. Masswe alitoa angalizo kwa wananchi miradi inakotekelezwa kuwa miradi hiyo itakapokuwa imekamilika huduma haitatolewa mpaka pale wananchi watakapokuwa wamemaliza kuchangia miradi hiyo ambayo wanantakiwa kuchangia asilimia 2.5 kwa kila mradi.
Imeandaliwa na:
Sylvester Raphael
AFISA HABARI
RS-KAGERA@2014

Next Post Previous Post
Bukobawadau