RAIS WA TFF MH.JAMAL MALINZI KUENDELEA KUWA MWENYEKITI WA (KRFA)
Mwenyekiti
wa chama cha mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera (KRFA)Jamal Emil Malinzi
akizungumza na Wajumbe waliojitokeza katika mkutano huo wa Utekelezaji
wa Chama cha Mpira wa Miguu (KRFA) Mkoa wa Kagera, Ambapo pia
alizungumzia swala zima la kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho,
Mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mkuu wa mkoa wa Kagera
Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera, Kanali Mstaafu Issa Njiku akizungumza na wajumbe
Pichani kushoto ni Bw. Christopher Kiiza, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji KRFA - TFF Kagera katikati ni Mkurugenzi wa
Sheria na utawala Shirikisho la soka nchini TFF Mdau Evodius Mtawala.
Chama
cha mpira wa miguu Mkoa wa Kagera (KRFA) kimefanya mkutano mkuu wa
kawaida kwenye ukumbi wa Mkuu wa mkoa wa Kagera na Mgeni rasmi alikuwa
ni Mkuu wa wilaya ya Missenye Kanal Issa Njiku.
Awali
akisoma taarifa yake mwenyekiti wa KRFA ambae pia ni Rais wa TFF Jamal
Emil Malinzi aliwashukuru wajumbe wote wa mkutano mkuu kwa namna
walivyoshiriki kwa namna tofauti katika kuendeleza michezo katika wilaya
zote za Mkoa wa Kagera,Hotuba iliyosheheni mipango kedekede ya kuinua
soka kwa ujumla nchini Tanzania na Kagera ikiwemo.
Katika
mambo mengi aliyoeleza ameweza kueleza changamoto nyingi zinazoikabiri
KRFA na kuwataka viongozi kuhakikisha wanawasiliana na Halimashauri za
wilaya zao kutenga maeneo ya viwanja vya michezo,akiongelea uwanja wa
Kaitaba amesema anayofuraha kuwajulisha wajumbe kuwa sasa uwanja huo
unawekewa nyasi bandia kwa ufadhili wa FIFA kwa asilimia mia moja,
Lakini pia amehaidi kuitisha Harambee ya wadau mbalimbali jijini Dar es
salam kwa ajili ya kupata pesa ya kujenga jukwaa moja katika uwanja wa
Kaitaba Bukoba.
Pia
aliweza kuelezea kuhusiana na nafasi ya Uenyekiti wa KRFA, Amesema tangu
amepata nafasi ya Rais TFF amekuwa akikutana na maswali mengi ya
waandishi wa habari na wadau kuhusiana na kujiudhuru nafasi hiyo,
(Wakati nakuja Bukoba nilikuwa na wazo ili la kujiudhuru, Lakini kila
mjumbe aliesimama hapa ameniomba nisijiudhuru mpaka wengine kutamka kuwa
iwapo nitajiuzuru basi nao watajiudhuru nafasi hii, lakini kuna mjumbe
kasema wapo watu wakati wa kampeni walikuwa wakisema natafuta nafasi hii
ili niweze kugombea urais, kwahiyo basi naomba nitamke kuwa
sitojiudhuru nitaendelea kuwa mwenyekiti wa KRFA.)
Katibu wa KRFA Saloum Umande Chama
Mdau A. Rutayuga, Mjumbe wa kamati Tendaji ya KRFA , Mjumbe wa mkutano mkuu wa TF
Mkurugenzi wa
Sheria na utawala Shirikisho la soka nchini TFF Mdau Evodius Mtawala .
Baadhi ya wajumbe wakipitia taarifa ya Utekelezaji ya Kamati ya Utendaji ya Chama cha mpira wa Miguu KRFA Mkoa wa Kagera
Mjumbe Ndugu Jacob Kilianga Kabaijo
Mwenyekiti wa BUFA Bw. Marick Tibabimale (kushoto) na Kulia ni Bw. Jerome Simon
Picha Na Faustine Ruta, Bukoba
BUKOBA fika ITEMBWE GENERAL SUPPLIES wakala mkuu wa Startimes ,wanapatikana Kashozi Road, mkabala na ofisi ya MAYAWA au piga simu namba 0787 007 666/0754 760 633.
Habari kubwa ni kwamba usipolipia unaweza kufurahia chanel 5 muhimu za nyumbani bure kabisa!!
STARTIMES ENJOY ULIMWENGU WA DIGITAL WA TANZANIA
.
.