KAMPUNI YA WATANZANIA WAZALENDO YAZALISHA MAWE YA DHAHABU MKOANI KAGERA KWA MARA YA KWANZA TANGU UHURU MWAKA 1961
Profesa Sospeter Muhongo Waziri wa
Nishati na Madini Akiwasili Katika Mgodi wa STAMIGOLD Biharamulo
Kuzindua Uzalishaji wa Tofali la Dhahabu la Kwaza lililozalishwa na
Kampuni ya Watanzania
Shimo la Kanda ya Magharibi Ambalo STAMIGOLD Wanachimba Dhahabu kwasasa.
Profesa Muhongo Akionyeshwa Ramani ya Uchimbaji wa Dhahabu Katika Shimo la Kanda ya Magharibi.
Profesa Muhongo Akikata Utepe Kuzindua Matofali ya Dhahabu Yenye Kilo 25 Katika Mtambo wa Kuchenjulia Dhahabu.
Profesa Muhongo na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Wakizindua Mawe ya Dhahabu na Kuyaonyesha mbele ya waandishi wa Habari
Picha ya Pamoja
Profesa Muhongo na Ujumbe aliombatana nao Wakitembelea Mtambo wa Kuchenjulia Dhahabu.
Na Sylvester Raphael
Shimo la Kanda ya Magharibi Ambalo STAMIGOLD Wanachimba Dhahabu kwasasa.
Profesa Muhongo Akionyeshwa Ramani ya Uchimbaji wa Dhahabu Katika Shimo la Kanda ya Magharibi.
Profesa Muhongo Akikata Utepe Kuzindua Matofali ya Dhahabu Yenye Kilo 25 Katika Mtambo wa Kuchenjulia Dhahabu.
Profesa Muhongo na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Wakizindua Mawe ya Dhahabu na Kuyaonyesha mbele ya waandishi wa Habari
Picha ya Pamoja
Profesa Muhongo na Ujumbe aliombatana nao Wakitembelea Mtambo wa Kuchenjulia Dhahabu.
Na Sylvester Raphael
Hatimaye
Kampuni ya Watanzania wazalendo STAMIGOLD yaandika historia nchini kwa kuanza uzalishaji
wa dhahabu katika mgodi uliokuwa ukijulikana kama TULAWAKA (African Barrick
Gold) uliopo Wilayani Biharamulo Mkoani Kagera ambapo tayari dhahabu ya kilo 25
tayari imezalishwa.
Uzalishaji
wa tofali la kwanza la dhahabu lililozalishwa na Kampuni ya
Watanzania STAMIGOLD lilizinduliwa jana tarehe 21/08/2014 na Waziri wa Nishati
na madini Profesa Sospeter Muhongo mgodini baada ya kutembelea na kujionea
shughuli mbalimbali za uzalishaji wa
dhahabu katika mgodi huo.
Akitoa
taarifa ya mgodi huo kwa Waziri Muhongo Meneja Mkuu Bw. Denice Sebugwao alisema
STAMIGOLD ilianza uchimbaji na uchenjuaji wa dhahabu tarehe 15/07/2014 katika
Kanda ya Magharibi na tayari mawe mawili ya dhahabu yamezalishwa yenye jumla ya
kilo 25.
Profesa Muhongo akizindua uzalishaji wa tofali la
kwanza la dhahabu alisema kuwa Kampuni ya STAMIGOLD ni Kampuni ya kwanza ya Watanzania kuzalisha
dhahabu nchini, alisema tangu amalize chuo kikuu mwaka 1979 hajawahi kuona
kampuni ya watanzania ikizalisha dhahabu.
Pia
waziri huyo wa Nishati na Madini aliipongeza Kampuni ya STAMIGOLD kwa kuajili
kampuni nyingine za Watanzania ili kukuza upeo mpana wa ajira. Kampuni
zinazofanyakazi na STAMIGOLD ni SUMA JKT katika ulinzi na Kampuni nyingine ya
kuchimba dhahabu inayoundwa na Wataalamu wa Kitanzania.
Profesa
Muhongo alitoa angalizo kwa Kampuni ya STAMIGOLD kuwa wachape kazi kwa nguvu siku zote kama walivyoanza na isifike
mahali wakazembea na kupelekea kuiua kampuni hiyo. Pia aliwahakikishia wafanyakazi kuwa wizara ya
Nishati na Madini itahakikisha kampuni hiyo inasimama daima.
Kwa
kuwa STAMIGOLD ni Kampuni ya Watanzania
Profesa Muhongo alisema kuwa serikali inataka kuonyesha mfano kupitia
kampuni hiyo kuwa Watanzania wanaweza kufanya kazi kwa ubora zaidi na kuzalisha
dhahabu itakayowanufaisha watanzania wote kwa ujumla.
Maagizo; Profesa Muhongo aliagiza wafanyakazi
wa STAMIGOLD kutoutumia mgodi huo kama sehemu ya siasa na harakati isipokuwa
uzalishaji wa dhahabu tu. Pia aliuagiza uongozi wa mgodi huo kuwasaidia
wachimbaji wadogo ili kuongeza ajira kwa vijana.
Bodi
ya STAMIGOLD iliagizwa kuwa watumishi
wote ambao wanakaimu wapewe madaraka kamili ili waweze kuchapa kazi kwa uhakika zaidi. Menejimenti ya mgodi huo ihakikishe inawalipa
wafanyakazi mishara mizuri ili kuongeza ufanisi wa kazi na ushindani katika
soko la wataalam. Mkuu wa mkoa wa Kagera naye aligizwa kuusimamia mgodi huo kwa
karibu sana.
Mkuu
wa mkoa wa Kagera Mhe. Massawe alimshukuru Profesa Muhongo na serikali kwa
ujumla kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo katika mkoa wa Kagera.
Alimshukuru Profesa Muhongo kwa kuisimamia vizuri wizara na kuliunda na
kulisuka upya shirika la STAMICO.
Pia
Mhe. Massawe alimhakikishia Profesa Muhongo kuwa ulinzi na usalama kuzunguka
mgodi huo utaimarshwa kwa kushirikiana na wananchi ili kusiwepo na uharibifu na
uvunjifu wa amani katika maeneo hayo.
Mgodi
wa STAMIGOLD unalengakuisaidia Jamii inayouzunguka mgodi huokwa kusaidia
shughuli mbalimbali za kijamii kama kukarabati barabara za vijiji
vinavyozunguka mgodi huo, kusaidia katika upande wa afya aidha kutengeneza na kugawa madawati katika
shule zinazouzunguka mgodi huo.
STAMICO
(State Mining Cooperation) ni shirika lililoanzishwa mwaka 1972 lengo likiwa ni
kuendeleza sekta ya Madini. Shirika hili liliundwa tena upya na serikali mwaka
2008 ili kulipa uwezo wa kufanya kazi iliyo kusudiwa hapo mwanzo.
STAMICO ina miradi
ambayo kwasasa inashughulika nayo ili kuleta faida kwa watanzania ikiwa ni
kampuni ya ndani. Miradi hiyo ni mradi wa STAMIGOLD Biharamulo, Mradi wa Madini
ya tini Kyerwa, Makaa yam awe Kiwira, Tanzanite Melalani, na Mgodi wa dhabu wa
Buhemba