WATU WANNE WAFARIKI KATIKA AJALI YA GARI WILAYANI MULEBA
Na mwandishi wetu
Muleba
WATU wanne wamefariki dunia na majeruhi wengine 14 katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Nundu-Katoke
wilayani Muleba mkoani Kagera baada ya
gari aina ya Toyota Hilux lenye namba za usajiri T832 lililokuwa linaendeshwa
na bwana Omar Twaha (40) kupinduka na
kupotea njia.
Hata hivyo Kamanda
wa polisi mkoani Kagera Agustino Ollomi alisema
kuwa tukio hilo lilitokea novemba 07 mwaka majira ya saa 1:10 jioni wakati watu
hao walipokuwa wakitoka msibani ndipo
walipofika eneo la Nundu katoke kutokana na mwendo kasi lililokuwa nalo gari
hilo lilipasuka tail la nyuma la kulia na kuacha kupinduka.
Ollomi aliwataja
waliopoteza maisha kuwa ni pamoja na Evodius ambaye amekufa papo hapo
aliyetambulika kwa jina moja ambaye mwili wake umehifadhiwa katika kituo cha
afya Kaigara, Diana Pius aliyefia katika hospitali ya Rubya, Edmundi Fidelis na
Renatus Vedasto miili yao imetunzwa katika hospitali ya Kagondo.
Alisema majeruhi watatu hali zao ni mahututi ambao ni Thobias
Titus (28) fundi wa vioo Rwamishenyi , Max Hanta (45) na Rweyemamu Frediricki wote wakazi wa Rwamishenyi ambao wamelazwa katika hospitali ya Kagondo na madakitari wanaendelea
kuwahudumia ili kuokoa maisha yao na
majeruhi wengine kumi na mmoja wanaendelea na matibabu katika hospitali ya
Kagondo.
Kamanda Ollomi
aliongeza kuwa , chanzo cha ajali hiyo ni kutokana na mwendo kasi wa huyo dreva na gari lilipata pancha taili
ya nyuma mkono wa kulia na baada ya
tukio dreva ametoroka na novemba 08 mwaka huu alikamatwa na atafikishwa mahakamani.
Hapo hapo, Perepetua Julius (32) amekutwa amekufa katika tarafa ya Rulenge wilayani Ngara baada ya kupigwa na kitu kizito
kichani.
Aidha Kamanda
huyo wa polisi mkoani Kagera Agustino Olomi alieza juu ya tukio hilo na kusema kuwa, marehemu amekutwa amekufa akiwa ametupwa kichakani
umbali wa mita 100 kutoka anapoishi.
Aliongeza
kuwa , mnamo novemba 04 mwaka huu majira ya saa nne usiku marehemu aliondoka
nyumbani kwake hakuonekana tena hadi alipokutwa amepoteza maisha novemba 07 mwaka
huu na uchunguzi umebaini kuwa alipigwa kitu kizito kichwani.
Amesema mtu
mmoja ambaye ni mume wa marehemu
aliyefahamika kwa jina la Julius Saimon Sengiyunva anashikiliwa na jeshi
la polisi kutokana na tukio hilo baada ya kuwepo ugomvi wa muda mrefu baina ya
marehemu na mume wake.