MAZIWA YA ASAS DAIRIES LTD NI MAZIWA BORA - WAZIRI MKUU KASIM MAJALIWA
BUKOBAWADAU
21 Jan, 2017
waziri mkuu Kasim Majaliwa akifurahia ubora wa maziwa ya Asas
Mkurugenzi wa kampuni ya Asas Bw Salim Abri akiteta jambo na waziri mkuu Kasim Majaliwa
Asas akimweleza jambo waziri mkuu Kasim Majaliwa
Waziri Mkuu Kasim Majaliwa akifurahi jambo na Bw Asas
Viongozi mbali mbali wakimsikiliza waziri mkuu
Waziri Mkuu akitoa maelezo kwa viongozi wa mkoa wa Iringa
Familia ya Asas wakifuatilia hotuba ya waziri mkuu
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya maziwa ya Asas Bw Fuad Abri akisoma taarifa ya kampuni hiyo mbele ya waziri mkuu
Wananchi wakifuatilia hotuba ya waziri mkuu Kasim Majaliwa
Waziri wa Nyumba ,ardhi na maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi akizungumza mbele ya waziri mkuu
waziri mkuu Kasim Majaliwa akifuatilia taarifa ya kampuni ya Asas ,wengine ni salim Abri na Waziri wa Nyumba ,ardhi na maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi
Farasi waliopo shamba la mifugo la Asas
Askari wa FFU Iringa wakitazama ng'ombe shambani kwa Asas
Nyati wanaofugwa shambani kwa Asas Iringa
Kundi la Nyati wanaofugwa shambani kwa Asas eneo la Igingilanyi Iringa
Askari wa FFU Iringa akipiga picha na nyati waliopo shambani kwa Asas
Asakari wa FFU Iringa wakitazama vifaa vya kuhamilishia ng'ombe
Ng'ombe waliopo shamba la Asas la Nduli
Msafara wa waziri Mkuu ukiondoka shambani kwa Asas
Waziri mkuu akishukuru kwa wenyeji kabla ya kuondoka
waziri mkuu Kasim Majaliwa akiagana na Salim Abri
Waziri mkuu akiagana na mkurugenzi wa kampuni ya maziwa ya Asas Fuad Abri
Waziri mkuu akitembelea shamba la mifugo la Asas
Bw Feisal Abri akimpa maelezo waziri mkuu Kasim Majaliwa
Waziri mkuu akiendelea kutembelea shamba la mifugo la Asas
Waziri mkuu Kasim Majaliwa akitazama ng'ombe ambao wanasubiri kupandikizwa mbegu
Zoezi la kuhamilisha ng'ombe likifanyika
Mtaalam akionyesha namna ya kupandikiza mbegu ng'ombe
Waziri Lukuvi kulia akiteta jambo na waziri mkuu
Mtambo wa maziwa
Waziri mkuu akifurahi majina ya ng'ombe za Asas
Zoezi la kukamua maziwa likiendelea
Waziri mkuu Kasim Majaliwa akisalimiana na Salim Asas baada ya kufika kutembelea shamba la mifugo katikati ni mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza
Waziri mkuu Kasim Majaliwa na viongozi mbali mbali wakielekea kutembelea shamba la mifugo ya Asas( picha na MatukiodaimaBlog)
Na MatukiodaimaBlog
WAZIRI mkuu Kasim
Majaliwa amepongeza kampuni ya maziwa
ya Asas
Dairies Limited kwa uzalishaji wa
bidhaa bora nchini na
kuwa ni kampuni pekee ambayo
inafanya vizuri katika utengenezaji wa bidhaa bora za maziwa
na kuwa imeweza kutekeleza kwa vitendo kauli
mbiu ya Rais Dkt John Magufuli
ya Tanzania ya viwanda .
Kuwa serikali itaendelea
kuiunga mkono kampuni hiyo ya
Asas ambayo pamoja na kufanya
vizuri katika ubora wa maziwa
bado ni kampuni yenye sifa nzuri ya ulipaji wa
kodi nchini pia ni kapuni ya mfano kwa ufugaji bora
wa ng’ombe
“ Nimefurahishwa na ufugaji
bora ufungaji wa
mifugo unaofanywa na Shamba la kampuni
ya Asas ya mkoani mkoani Iringa ni mzuri
sana lazima wafugaji wengine
nchini kufika kujifunza jinsi ya ufugaji
.”
Alisema
kuwa bidhaa zinazotengenezwa na kampuni ya Asas Dairies kama mtindi
unaozalishwa na kampuni hiyo ya Asas ni mzuri na hata ukinywa hauna
hofu ya kuharisha kama mtindi inayotengenezwa na wengine
Akizungumza leo
wakati wa ziara yake ya kutembelea
shamba la Asas lililopo eneo la Igingilanyi katika
wilaya ya Iringa ,waziri mkuu
alisema kuwa amefurahishwa na
ufugaji unaofanyika katika eneo hilo na kutaka watu
wengine kuanza kufuga mifugo badala ya kuwa
wachungaji wa mifugo .
Kwani alisema tatizo
kubwa ya migogoro kati ya
wachungaji na wakulima
inasababishwa na baadhi ya watu kuendesha uchungaji
wa mifugo badala ya kufuga
na hivyo kupelekea kugombea maeneo ya kuchungia
huku wakulima wakivamiwa na wachungaji hao .
Alisema kwa lengo la
kukomesha migogoro kati ya
wachungaji na wakulima anawaagiza
maofisa mifugo kote nchini
kuanza kuitambua mifugo
yote na kuiweka alama maalum
itakayosaidia kutambua eneo ambalo
mifugo hiyo inatoka na itakuwa ni njia ya kukomesha wachungaji kuhama hama
Hivyo alisema ni
mhimu sana kwa
maofisa Mifugo katika Halmashauri zote nchini
kuanza kutoa elimu kwa
wafugaji ili kuondokana na kuwa
na mifugo mingi isiyo bora
na badala yake kuachana na uchungaji wa
mifugo na kujikita na ufugaji .
Alisema kuwa kwa
upande wa Halmashauri za
wilaya zote nchini
zinapaswa kuwapimia na kuwapa
hati ya umiliki wa ardhi
wawekezaji wote wakubwa
waliopo katika maeneo yao
lengo likiwa ni kuondokana na migogoro ya ardhi .
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI
BUKOBAWADAU
Bukoba Wadau ni mtandao unao toa habari na matukio yanayo tokea katika mji wa bukoba pamoja na mkoa wa kagera kwa ujumla.
Email:bukobawadau@gmail.com | Phone :Mc baraka:0784 505045, 0754 505043
Instagram @bukobawadau | Facebook @bukobawadau