Bukobawadau

BREAKING NEWS: SENENE WAMIMINIKA MANISPAA YA BUKOBA ASUBUHI YA LEO

Baadhi ya akina mama wakinunua senene.Kama anvyoonekana mama huyo akiwauzia senene,huo mfuko ulikua unauzwa kwa Tshs 400 tu.
vifurushi vya senene vikiwa vimewekwa chini tayari kwa kuuzwa,huku kwetu tunaita KAVERO
Senene wakipimwa kwa kiganja,kila kiganja kimoja ni miambili tuu.haya ushindwe wewe mdau.
Sehemu hii imechangamka kwa sababu senene wapo wengi,kama inavyoonekana katika picha wadau wakitafuta sehemu yenye bei nafuu.kulia bwana mdogo huyo sikuweza kupata jina lake mara moja alikua akiokota senene wanaoruka maeneo hayo.
Kwa mbali kabisa katika picha,soko la senene limechangamka.kweli kabisa"ensenene nenula kushaga enyama" PICHA NA MPIGA PICHA WETU
Next Post Previous Post
Bukobawadau