HABARI MUHIMU:mtoto wa ghadafi ameuwawa.
PICHA HII NI BAADHI TU YA MADHARA YA MAKOMBORA KWENYE NYUMBA YA MTOTO WA GHADAFI.
Serikali ya Libya imesema kuwa mtoto wa Kanali Ghadafi,Seif amehuwawa mjini Tripoli,pamoja na wajukuu watatu,katika shambulio la ndege za NATO.
HILI NI KOMBORA AMBALO ALIKUWEZA KULIPUKA BAADA YA SHAMBULIZI LA NATO.
Msemaji wa serikali ya Libya,Moussa Ibrahim ameeleza kuwa kiongozi wa Libya mwenyewe amesalimika katika tukio hilo kwenye nyumba alipokuwa akihishi mwanawe Seif Al-Arab Ghadafi.
Msemaji anasema shambulio hilo ni ushahidi wa wazi kuwa sasa kiongozi wa libya na familia yake wanalengwa.
Anadai kuwa Kanali Ghadafi na mkewe walikuwemo ndani ya nyumba hiyo wakati wa shambulio hilo,lakini ni shida kuona vipi aliweza kunusurika bila ya kujeruhiwa katika uharibifu wa makombora matatu yaliyo angushwa papo kwa papo.
NATO punde tu kwenye tarifa yake inasema ililenga pahala pa uongozi wa shughuli za kijeshi,haikulenga mtu maalum,lakini inasikitika kuwa kuna watu wamekufa.