Bukobawadau

Jenerali wa Rwanda akutwa na hatia


Aliyekuwa mkuu wa majeshi wa Rwanda Augustin Bizimungu amepewa hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela kwa kuhusishwa na mauaji ya kimbari mwaka 1994.

Mahakama ya kimataifa ya kusikiliza kesi za mauaji hayo ya Rwanda iliyopo nchini Tanzania pia imemhukumu Augustin Ndindiliyimana aliyekuwa mkuu wa majeshi ya polisi, lakini ameachiwa kutokana na kwamba tayari ametumikia kifungo hicho.

Majenerali wengine waandamizi nao wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kila mmoja.

Takriban Watutsi 800,000 na Wahutu wenye msimamo wa wastani walifariki dunia katika mauaji hayo ya kimbari yaliyochukua siku 100.

Bizimungu na Ndindiliyimana ni miongoni mwa viongozi waandamizi waliohukumiwa kwenye mahakama hiyo ya ICTR, iliyoundwa kusikiliza kesi za watu waliofanya uhalifu wakati wa mauaji hayo.

Mahakama hiyo ilisema, Bizimungu, aliyekamatwa Angola mwaka 2002, alikuwa amewadhibiti vizuri wanajeshi wake mwaka 1994.

Hata hivyo, Ndindiliyimana, inasemwa alikuwa na "udhibiti mdogo" juu ya majeshi yake na alielezwa kupinga mauaji.

Next Post Previous Post
Bukobawadau