Bukobawadau

Mkuu wa IMF ameshtakiwa New York

Polisi mjini New York wamemshtaki mkuu wa Shirika la Fedha Duniani, IMF, Dominique Strauss-Kahn, kwa kujaribu kumbaka mtu na kumzuwia.
Mashtaka hayo yanahusu msichana mfanyakazi wa hoteli chumbani alimokuwa akikaa Bwana Strauss-Kahn.

Wakili wake amesema atakanusha mashtaka hayo.

Bwana Strauss-Kahn, alikamatwa ndani ya ndege kabla ya kuondoka kuelekea Ulaya.

Dominique Strauss-Kahn, mkuu wa IMF, hivi sasa yuko kati-kati ya juhudi za kuziokoa nchi za Umoja wa Ulaya zenye matatizo ya fedha.

Mwaka wa 2008, alichunguzwa na bodi ya IMF, kuhusu uhusiano wake na mwanamke aliyekuwa piya mfanyakazi wa IMF.

Hakutolewa kazini, lakini iliamuliwa kuwa alionesha "ukosefu mkubwa wa busara".

Anakanusha tuhuma kuhusu tukio lilotokea jana mjini New York, lakini ni wazi kuwa tukio hilo litamuandama, na linaweza kuathiri imani ya watu juu yake katika majadiliano yoyote atayofanya.

Alikuwa yuko njiani kwenda Ujerumani, kukutana na Kansela Merkel.

Mada ya mazungumzo haikufichuliwa, lakini inajulikana kuwa hali ya uchumi wa Ugiriki imekuwa kwenye mawazo ya duru za kifedha.

Next Post Previous Post
Bukobawadau