Bukobawadau

Rais Museveni kuapishwa leo

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni,anatarajiwa kuapishwa kwa muhula mwengine hii leo siku ya Alhamisi.Anaapishwa huku kukiwa na wingu la shutma kwa utawala wake kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya upinzani.
Rais Yoweri Museveni
Katika siku za hivi karibuni serikali imelaumiwa kwa namna walivyokabiliana na maandamano ya upinzani na kusababishwa kulazwa hospitali kwa mwanasiasa wa upinzani, Dk Kizza Besigye pia kumezua shutma kali.

Wakati atakapoapishwa kwa muhula mwengine,Yoweri Museveni atakuwa amejiongezea muda wa kukaa madarakani kwa takriban miaka thelathini.

Alipoingia madarakani mwaka 1986 alisema tatizo la viongozi wa Afrika ni kukaa kwenye utawala kwa muda mrefu sana.

Kwa miaka mingi amefanya juhudi kuijenga upya nchi ya Uganda baada ya nchi hio kuwa kwenye vita na utawala mbaya.

Bado anaungwa mkono na wengi lakini wadadisi wanaona kuendelea kutegemea jeshi kunaweka nchi hio katika mazingira magumu.
Kizza Besigye akikabiliana na polisi,na picha ya juu ni kipindi yupo hospitalini.
Upinzani umekabiliwa vibaya katika wiki za hivi karibuni. Kiongozi wa upinzani, Dokta Kizza Besigye,bado yuko nchini Kenya baada ya kupata matibabu kufwatia kushambulia kwake na polisi.

Mapema siku ya Jumatano,Besigye alisema kuwa alizuiwa kupanda ndege kutoka Nairobi kwenda Uganda, baada ya kupatiwa matibabu nchini Kenya.

Serikali ya Uganda imekanusha kumzuia kusafiri.

Haijulikani kama atajaribu kusafiri hii leo kwenda nyumbani wakati Rais Museveni anaapishwa - hatua ambayo italeta aibu kwa serikali.

Baadhi ya viongozi walioalikwa kwa sherehe za kuapishwa kwa Rais Museveni waliwasili Kampala siku ya Jumatano huku wengine wakitarajiwa hii leo siku ya Alhamisi.

Next Post Previous Post
Bukobawadau