Bukobawadau

WASIFU WA OSAMA BIN LADEN

Osama bin Laden alizaliwa mwaka wa 1957, katika familia ya kitajiri nchini Saudi Arabia.
Osama bin Laden

Ana zaidi ya ndugu na dada 50. Babayake Osama alimiliki kampuni kubwa ya ujenzi. Katika baadhi ya picha zake za utotoni, Osama ameonyeshwa akiwa amevalia mavazi ya kifahari na ya gharama kubwa, akiwa likizo katika miji mbali mbali barani Ulaya.

Hata hivyo mwanzoni mwa miaka ya themanini alitapa mgongo maisha haya ya kifahari na kitajiri na kujiunga na vuguvugu la kupigania haki dhidi ya utawala wa Kisovieti baada ya majeshi yake kuishambulia Afghanistan.

Wakati huo, akipigana pamoja na Waarabu wenzake, alizindua kundi la kigaidi la Al Qaeda. Mnamo mwaka wa 1998, alitangaza fatwa yaani vita vikali vya kidini dhidi ya Marekani. Osama alisema alikasirishwa na hatua ya Marekani kuweka majeshi yake katika ardhi ya Kiislamu, katika nchi mbalimbali Mashariki ya Kati.

Alioa mke wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 17 na baadaye akawaoa wake wengine wanne.
Osama Bin Laden anaaminika kuwa na watoto 17

MWILI WA OSAMA BIN LADEN BAADA YA KUFIKWA NA MAUTI.picha hii hapo chini ni kwa mujibu wa vyanzo vya tovuti yetu.bukobawadau.blogspot.com
Maiti ya Osama Bin Laden baada ya shambulio la risasi

Na tayari mazishi yake yamefanyika lasmi nchini marekani.

Huku Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akisema ni simanzi kubwa kwa walio ondokewa na ndugu yao,na ni huzuni mkubwa kwa familia ya Osama Bin Laden na akasema ni faraja kubwa kwa maaduhi zake.Kikwete ameyasema hayo wakati akijibu swali alilo ulizwa kwamba ni vipi ameuchukulia kifo cha Osama Bin Laden.
Next Post Previous Post
Bukobawadau