Bukobawadau

Kituo Cha Hija Nyakijoga Jimbo katoliki la bukoba... Kama anavyo tujuza Mc.

Ivi karibuni waumini wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Tanzania, waliadhimisha Jubilee ya miaka hamsini ya kituo cha hija cha Nyakijoga, kilichoanzishwa na hayati Kardinali Laureani Rugambwa alipokuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Rutabo, kama kumbukumbu ya miaka mia moja, tangu, Bikira Maria amtokee Mtakatifu Bernadetha kule Lourdes, nchini Ufaransa. Bikira Maria alimdhibitishia Bernadetha kwamba, Yeye alikuwa amekingiwa dhambi ya asili, ili kushiriki katika mpango wa ukombozi.
Bikira Maria akawa ni Tabernakulo ya Kwanza, ili aweze kumzaa Neno wa Mungu aliyefanyika mwili, kwa njia ya Roho Mtakatifu, akawa mwanadamu. Sherehe hizi zilikwenda sambamba na maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 150 tangu Bikira Maria amtokee Mtakatifu Bernadetha, shereheke ambayo hivi karibuni, ilihitimishwa kwa ziara ya Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita nchini Ufaransa.

Maji ya baraka yakimiminika
Kituo hiki kilianza 1954 kama kituo cha Hija cha Parokia ya Mugana, hapa tulipo.
Wakati huo Parokia ya Mugana ilikuwa ikijiandaa kuadhimisha Jubilei ya Miaka 50 tangu ilipoanzishwa. Jubilei ilikuwa iadhimishwe mwaka 1955. Kituo hiki cha Hija kilianzishwa kwa madhumuni ya kushiriki kiroho katika maadhimisho ya Jubilei ya miaka 100 tangu tamko rasmi la Kanisa, la mwaka 1854, kuwa ni nguzo ya imani kwamba Bikira Maria aliumbwa bila dhambi ya asili. Vilevile, mwaka 1958 kuliadhimishwa Jubilei ya miaka 100 tangu Bikira Maria mwenyewe alipomtokea msichana Bernadeta Subiru huko Lurdi Ufaransa mwaka 1858 na kujitambulisha kuwa yeye ndiye “aliyeumbwa bila dhambi ya asili”

Ni juu ya Nyakijonga,na hospitali ya Mugana,Iliopo chini ya Parokia ya Mugana bila shaka wadau wengi mmebahatika kufika hapo,kama si kutembea basi ni kwa matibabu au Hija.Alikadhalika wengine mmesoma maeneo hayo ya shule ya msingi Mungana na kama alivyo kutwa mzee huyo katika Picha na camera ya wadau akiwa chakari ni kielelezo tosha juu ya kile kinacho itwa kwa lugha ya kihaya:(kalinya)!!!!!Habari na Picha by Mc.
Next Post Previous Post
Bukobawadau