MBOWE ;kinachogomba sio posho tu za wabunge ni posho za watumishi wengi serikalini
Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa malipo ya wabunge yamegawanyika katika sehemu nne ambazo ni pamoja na mshahara ambao ni Sh 2,300,000 kwa mwezi, posho ya ubunge kila mwezi ambayo ni Sh 5 milioni, posho ya kujikimu (per-diem) Sh80,000 wawapo nje ya majimbo yao kikazi na posho ya vikao (sitting allowance) ambayo huwa ni Sh70,000 kwa kila mbunge.
Kwa maana hiyo, kwa kawaida mbunge hulipwa Sh 7.3 milioni kila mwezi kabla ya kukatwa kodi na wawapo Dodoma na Dar es Salaam kwa ajili ya vikao vya kamati za bunge au mikoani kwa ajili ya kukagua shughuli zilizopo chini ya kamati zao. Hulipwa kiasi cha Sh150,000 kila mmoja kwa siku ambazo ni Sh 70,000 kwa ajili ya vikao na Sh 80,000 kwa ajili ya kujikimu.
Kwa maana hiyo bunge linatarajiwa kutumia kiasi cha Sh1.788 bilioni kwa ajili ya kugharamia vikao 73 vya Bunge la Bajeti iwapo wabunge wote 350 waliopo watahudhuria vikao hivyo.
Kwa hesabu hizo, kila mbunge katika mkutano wa Bunge la Bajeti anatarajiwa kuondoka na kitita cha Sh5.1 milioni mbali na Sh 5.58 milioni ambazo ni malipo kwa ajili ya kujikimu, fedha ambazo ni mbali na mshahara wake kwa mwezi na posho ya ubunge.
Wakati yote haya yakiendelea Mbunge wa kigoma kaskazini (chadema)Zitto Kabwe amesema yupo tayari kufukuzwa bungeni kwa ajiri ya kukataa posho.. habari by Mc