Wasichana wapimwa Bikra nchini Misri
Shirika la kutetea haki za binaadam la Amnesty International limeitaka serikali ya Misri kufanya uchunguzi kamili baada ya maafisa wa juu wa kijeshi kukiri kuwa waliwafanyia vipimo vya ubikira, wanawake waliokuwa akiandamana hivi karibuni.
Amnesty imetaka wote waliohusika kufikishwa mbele ya sheria.
Tuhuma hizo ambazo zinadaiwa kutokea kwa wanawake waliokuwa wakiandamana baada ya kuondoka madarakani kwa rais Hosni Mubarak zimewashitusha wengi nchini Misri.
Misri
Waandamanaji wanawake katika hali ya mwamko wa mageuzi nchini misri
Kwa mujibu wa Amnesty International, wanawake 18 walikamatwa, kupigwa na kupigwa shoti za umeme baada ya wanajeshi kusambaza waandamanaji katika eneo la wazi la Tahrir mwezi machi.
Wanawake wote hao isipokuwa mmoja tu, walivuliwa nguo, kulazimishwa kupimwa kama bado ni bikira na kutishiwa kushitakiwa kwa makosa ya ukahaba.
Kilichowashangaza wengi hasa ni matamshi ya Jenerali wa kijeshi mwenye cheo cha juu kukiri kuwa vipimo vya ubikira vilifanywa.
"Hawa wanawake sio kama mwanao au mwanangu wa kike. Hawa ni wasichana walioweka kambi katika mahema na waandamanaji wa kiume."
Jenerali huyo ameongeza kusema: "Hatukutaka waje kusema tumewanyanyasa kijinsia au kuwabaka, kwa hiyo tulitaka kuthibitisha kuwa wao sio mabikira."
Suala hili linaonesha jinsi mvutano unaoendelea kati ya baraza la kijeshi ambalo linatawala Misri na vijana wanaoandamana ambao walisababisha kuondoka kwa Rais Mubarak.