Bukobawadau

BALOZI HAMIS KAGASHEKI AWAHUTUBIA WADAU MJINI BUKOBA:Ushuru,kodi na Sukari vyaonekana Kero kubwa

Balozi kagasheki mda mchache baada ya kufika kwenye eneo la mkutano na kusalimiana na wadau mbalimbali kabla ya kuanza kuwahutubia na kusikiliza pia kero zao.


Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini na Naibu waziri wa wizara ya mambo ya ndani Balozi Hamis Juma Sued Kagasheki akiwahutubia wananchi wake amesema;Pamoja na shughuli ya Bunge inayoendelea mjini Dodoma na moto unaowaka Bungeni ameona ni vyema kwake kujaribu kupata muda wa kuongea na wadau kwa sababu nako pia kuna kero, maneno na chokochoko za hapa na pale.

Pia Balozi Kagasheki amesema mojawapo ya kero kubwa zinazowasibu wakazi wa manispaa ya Bukoba ni swala zima la ulipaji wa kodi na ukusanyaji wa ushuru halikadhalika upimaji wa viwanja vipya na ukizingatia kuna watu walilipia viwanja halmashauri ila kutokana na ubabaishaji wa uongozi uliokuwepo madarakani basi watu hao hawakuweza kupata viwanja hivyo ama kurudishiwa pesa zao,Akionyesha kuguswa sana na swala hilo Mh Balozi Kagasheki amesema manispaa imekwishapata sh 1.6 bilion kwa ajili ya upimaji viwanja vipya 5000 na atahakikisha wale wote waliolipia viwanja wanapewa haki yao.Pia aliongeza kuwa kuna fidia mara mbili yaani fidia ya mazao, miti na fidia ya ardhi.

Pia Balozi amesema kuna haja kubwa ya kuangalia kasi ya maendeleo ya mkoa wetu kwa kutoa mfano kwamba wakati nchi hii inapata uhuru mkoa wa Kagera ulikuwa wa nne kimaendeleo lakini hivi sasa mkoa huu ni wa tatu kutoka mwisho

Kuhusu kero za ndani ya soko na ushuru unaotozwa, Balozi Kagasheki amelitolea ufafanuzi na kunukuu baadhi ya maneno ya Waziri wa fedha Mh Mkulo ya kwamba juu ya kutafuta vyanzo vya mapato vya Halmashauri na Manispaa imefanyika marekebisho na kutoza sh 50 kwa kila aina ya Bidhaa.

Na amesema kwamba sheria hiyo ni kwa bidhaa zinazositahili na ambazo siyo vipodozi,ndizi au banana na akamaliza kwa kusema ni swala la madiwani kuona ni bidhaa zipi zinazostahili na akakoleza kwa neno la Kihaya kwamba(mwashobokelwa)akimaanisha kama wadau wamemuelewa.


Wakati yote hayo yakiendelea wananchi wametoa dukuduku lao kwa kutishia kuacha kununua sukari inayozalishwa na kiwanda cha Kagera sugar kutokana na kupanda kwa bei ya sukari kutoka sh 1600-2000
wadau wa Bukoba wamedai kuwa kutokana na kupanda kwa bei wafanyabiashara walikua wakinunua sukari Mjini Jinja nchini Uganda na kuiuza hapa kwa sh 1500 kwa kilo 1 lakini maofisa wa mamlaka ya mapato wa Kyaka na Mtukura wameanza kutoza sh elfu 80 kwa kila mfuko wa sukari inayotokea Uganda kitendo kinachosababisha bei kuwa juu na wamemwomba mbunge kulifanyia kazi swala hilo.

Balozi Kagasheki akiongea juu ya swala zima la kujivua gamba ameonyesha kushangazwa na kauli hiyo na kusema yeye hajui na haoni maana ya neno 'Kujivua gamba' na amewaasa wadau wa Bukoba kuwa hiyo ni siasa ya ubinafsi na wasikubaliane nayo kabisa,kwa msingi kwamba yeye kinachomuhusu ni matatizo ya wananchi si vinginevyo pia amesema hajawahi kuona duniani kote chama kinapata Jimbo halafu kinaliachia kwa sababu ya maneno ya kujivua Gamba ,yeye hakubaliani na hali hiyo na yupo tayari kutofautiana na yeyote yule katika swala lenye masilahi kwa wananchi hata kama yeye yumo serikalini.

Pia Balozi Kagasheki amesema alishangazwa na mkutano wa wana ccm wenzake uliofanyika Jijini Mbeya juma lililopita ambapo Mh Sitta na Mh Mwakyembe walionyesha kufanya kampeini za urais mwaka 2015

Pichani ni wazee wadau wa mji alhaji Kagire na Mzee Hudi.

Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya bukoba kushoto ni Mh Bigambo Mh Bigambo diwani kata ya Bakoba (CUF)|

Wadau mbalimbali wakimsikiliza kwa umakini Mbunge wao Balozi Kagasheki Naibu waziri wizara ya mambo ya ndani,hii leo.


Balozi Kagasheki akiendelea kuhutubia wadau.

Pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mh Samwel Kamote

Pichani ni Ndg Bagoka akiuliza swali kwa naibu waziri wa mambo ya ndani Balozi Kagasheki juu ya mauwaji ya assecdo ya pikipiki yanayojitokeza mara kwa mara
Pamoja na wadau wengine katika pPicha ni Ernest Nyambo(mkuu wa bandari)akifatilia maneno ya balozi kwa kina.
Mwanamama mfanyabiashara wa sokoni Bukoba akijaribu kumwonyenya Mh Mbunge daftari lake la mauzo ya kila siku na kile anachokipata na kutoa hoja yake ya ushuru ulivyo juu kwamba hauendani na hali ya biashara ilivyo.

< b>Haya yote kiujumla ndio yaliojiri kama anavyotueleza shuhuda wetu Mc.
Next Post Previous Post
Bukobawadau