Bukobawadau

HAPA NA PALE KATIKA MATUKIO.


Wanafunzi wa Darasa la Saba ambao wanajiandaa na mitihani ya taifa ya kumaliza elimu ya shule ya msingi Manda wilaya ya Ludewa wakivua dagaa katika Ziwa Nyasa muda wa masomo baada ya kufukuzwa shule kwa kushindwa kulipa mchango wa shilingi 600 kila mmoja kwa ajili ya kuchangia chakula cha walimu wanaofika kusimamia mitihani ya kujipima ya Kata ya Manda. Hali ya uchumi duni ya wananchi wa vijijini ni chanzo kikubwa cha wazazi wao kushindwa kulipa kiasi hicho cha fedha.
Picha na Francis Godwin


PICHANI: Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP..., Said Mwema akivishwa helmet baada ya Taasisi ya Helmet Vaccin Initiative Tanzania, kukabidhi msaada wa helmeti 500 kwa jeshi hilo wakati wa hafla ya uzinduzi wa uhamasishaji jamii kuvaa kofia hizo wakipanda pikipiki; Dar es Salaam leo katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)

Katika hali isiyo ya kawaida na yakushangaza njemba hizi bila woga wala aibu ziliendelea kupiga kilaji katikati ya maji after Rain,hebu mdau tuelezee katika maoni unalifikiliaje swala hili katika kujenga taifa letu?
Next Post Previous Post
Bukobawadau