Bukobawadau

Manispaa Bukoba hii hali vipi tena?!!!!!!!!!-By Mc

Wakati miji,manispaa na Majiji mbalimbali nchini yakiwa katika ushindani wa kuakikisha usafi ni sehemu ya mipango endelevu,hali hiyo pia inaendelea hapa manispaa ya Bukoba ukizingatia ni mda mchache toka mji wetu umepata msaada toka UN habit wa magarina matrekta kwa ajiri ya kubebea takataka.

Cha kushangaza ni leo hii majira ya saa tano asubuhi camera ya wadau tumeshuhudia gari moja la Manispaa likiwa limebeba takataka uku zikidondoka barabarani kana kwamba barabara ni mbovu hivyo gari limeshindwa kuimili mzigo hama watumishi hao wa Umma awakuona kinacho endelea.Tukio hilo kwa kiasi limeleta hisia tofauti kwa wadau
.
Mwonekano wa Msikiti wa Jamia jirani kabisa na lilipotokea tukio hili na wahusika kutokujari chochote mpaka camera yetu inafika hapo ni kitendo ambacho sichakistarabu!!!!!!
Makutano ya barabara ya Jamhuri jirani kabisa na kwa Kagambo ndio mwanzo wakitendo hiki kama unavyo jionea mdau.
Next Post Previous Post
Bukobawadau