OGOPA KITU KUPENDA:........ni matamu na yana sumu kali!!!!!!!!!!!!!!!!!
Ni ukweli usiopingika kuwa mapenzi ni matamu sana pale panapokuwa na maelewano na maridhiano baina ya wapendanao lakini mapenzi hayo hayo huwa sawa na sumu kali inayoua pale mambo yanapokuwa kinyume, mfano halisi ni mwanamke huyu wa nchini China ambaye aliokolewa sekunde ya mwisho kabla ya kujiua kwa kujirusha toka ghorofa ya saba baada ya bwana harusi wake kumkimbia na kwenda kumuoa mwanamke mwingine siku moja kabla ya harusi yao