Bukobawadau

ZIARA YA RAIS WA JAMHURI YA MUHUNGANO WA TANZANIA DR.JAKAYA MRISHO KIKWETE MJINI BUKOBA.By mc

Hivi ndivyo Camera ya wadau ilivyo kuwa makini kwa kila kile kilichokuwa kikiendelea, Na hapo Mh Rais JK akishuka kwenye Ndege mara tu baada kukanyaga ardhi ya manispaa ya Bukoba.

Rais Kikwete akisalimiana na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba Dr. Anatory Aman ambaye ni Diwani wa kata ya Kagondo.

Mapokezi yaliambatana na Burudani ya Ngoma kutoka kwa kikundi cha Lugoloile.

Rais Kikwete baada ya kusaini kitabu cha Wageni Uwanja wa Ndege.
Safari ya kutoka uwanja wa ndege ilivyo anza mpaka kwenye shughuli moja wapo ya ufunguzi wa Hotel ya Cofee Tree Inn iliopo Manispaa ya Bukoba.
Hotel hii inamilikiwa na Chama cha Ushirika cha wakulima wa Wilayani Karagwe(KDCU)

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa ufafanuzi kwa wadau juu ya maswala ya Ushirika kwenye ufunguzi wa Jengo la hotel ya Cofee Tree Inn.
Mwonekana wa vyumba vya hotel ya Coffee

Dr. Jakaya wa kwanza kushoto,akifatiwa na Mzee Galiatano,Pia Mzee Muhamed Babu Mkuu wa Mkoa wa Kagera na wa Mwisho ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi(mbunge)Mama Anna Tibaijuka.

BAADA YA UFUNGUZI WA JENGO LA HOTEL YA COFFEE TREE INN MOJA KWA MOJA CAMERA YA WADAU ILIONGOZANA NA MSAFARA WA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE MPAKA KWENYE VIWANJA VYA JIMKANA AMBAPO SHUGHULI KUBWA ILIKUWA NI KUFUNGA MAADHIMISHO YA SIKU YA USHIRIKA DUNIANI,AMBAYO KITAIFA YALIFANYIKA MKOANI KAGERA.
Rais Jakaya akikaguwa banda la Maonyesho

Pichani ni Katibu wa Vijana CCM wilaya ya Bukoba Ndg Didas Zimbile akisalimiana na mdau Ndg Wilbload Peter Kahigi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wadau Mjini Bukoba katika maadhimisho ya kumi ya siku ya Ushirika Duniani.
Next Post Previous Post
Bukobawadau