Bukobawadau

HAPA NA PALE NA CAMERA YETU:Waitafuta Bukobawadau Wapate kuujuwa Mji Wa Bukoba!!!!

Wanaonekana katika hali ya Sintofahamu,wakiwa hawana ili wale lile..wakiwa na Mizigo mikubwa kwenye pikipiki zao za aina yake Moja BMW na nyingine HONDA hawa ni Waitaliano wakiwa kwenye Tour.
Ndipo jitiada zao zilipowakutanisha na Bukobawadau Blogspot na kuweza kulikabili jukumu la kuwazingusha viunga mbalimbali katika Mji Wa Bukoba,Wakionekana wenye hali ya Uchovu wakaomba niwatafutie Sehemu ya Kuegesha kabla ya mambo yote

Kitendo Bila Kuchelewa nikawapeleka moja kwa moja WarkGard Hotel mojawapo ya Hotel nzuri na ya kisasa Mjini Bukoba

Baada ya kufika ikawa ni swala la kubadlishana mawazo na kuojiana ni kwa nini nimeonelea na nimependelea sehemu hii

Sababu kadha wa Kadha zikatolewa ikiwa nipamoja na location ilipo Hotel hii,ubora wa huduma na View usawa wa Ziwa Victoria, naamini ata wewe msomaji mdau tungeweza kuelewana

Nikiwa na Mr Pietro Averono nje ya Hotel ya WarkGard na hapo tukajadili mawili matatu na kupeana miadi ya kuonana Usiku baada ya kazi huyo ndiye Mc Baraka!!
Pita pita usiku ilikuwa Maeneo ya Kolping Hotel

Usiku nikamsogeza mmojawapo Pande za Coffee Tree Inn kama unavyoweza kujionea

Kama Zali kiwanja hiki nikamkuta mdau Mkubwa wa Maswala ya Utalii Mr Willy(Kiroyera) akaweza kubabadua baadhi ya Mambo.
Camera yetu ikakutana na Mdau wa Siku nyingi,yeye kimaisha yupo Afrika Kusini ni Mr Evodius Lutemba maarufu kwa jina la(Mlokozi)
Next Post Previous Post
Bukobawadau