Bukobawadau

MATUKIO KATIKA DUA YA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA WA KIISILAMU 1433HIJIRIYA

Msikiti mkuu wa Ijumaa bukoba municipal ilipofanyika dua maalumu ya kuuaga mwaka wa kiisilamu uliopita 1432H na kuukaribisha mwaka mpya 1433H Dua imesomwa leo hii jumamosi tarehe 26/11/2011 sawa na tarehe 01 muharamu 1433
Bi Rukiya Abdallah Kabyemela na mdogo wake Yunusu Kabyemela nao walihudhuria dua
SHEIKH HARUNA ABDALLAH KICHWABUTA
Akitoa waadh kuhusiana na mwaka mpya wa kiisilamu 1433Hijiriya,pamoja na mambo mengine Sheikh waliwaasa waisilamu kuacha tabia waliyonayo sasa ya kila muisilamu anapopata elimu kidogo tu anaanzisha kundi lake dogo kwa masilahi yake binafsi kitendo kinachosababisha kurudisha maendeleo ya uisilamu nyuma,aidha aliongeza kwa kusema kuwa mwaka huu mpya kwa waisilamu ni mwaka unaotaka vitendo zaidi kuliko maneno ili kuweza kuendeleza gurudumu la waisilamu,aidha ameonya kuhusu wale wanaofurahia kumaliza mwaka sheikh amesema sio kweli kwani kila mwaka unoisha unakumaliza wewe kwa kupunguza umri wako na sio wewe unayeumaliza,sheikh alimaliza hotuba yake kwa kusisitiza umoja bila madhehebu na itikadi zinazowagawa waisilamu

Amir wa jamaati ya khuruuji fiiysabilillah na bilali wa msikiti wa bilele Ustadh Rajabu Omari(BOB RAJA)Akisikiliza waadh wa sheikh kwa makini sana.
Jembe namba one la Bukoba wadau Salumu Sadick Galiatano akisikiliza waadh kwa makini
Aamina....Aamina......Amina, Hshimu Mugurazi alisikia akiitikia dua.
Alhaji Fikira Kisimba
Wanafunzi wa madrasatil Fauzi wakiomba dua kwa pamoja

Wadau pichani ni Abdul Mugulazi na Badru Kagasheki
Pichani Kushoto waliosimama Ustadh Abdallah Adamu,Sheikh Haruna Kichwabuta,Alhaji Ayubu Alli Kagire,Ustadh Seifu Hussein, Mzee Uledi Sessango na Amini Idrisa aliyekaa chini
Next Post Previous Post
Bukobawadau