Bukobawadau

TUNATOA PONGEZI KWA UONGOZI NA WANACHAMA WA ONE BUKOBA ONE DESTINY:juu ya ufunguzi wa UShirika huo hiyo jana 12-11-2011.Bukobawadau tumeguswa sana na hotuba ya ufunguzi!!!!!!!


Mdau mwanzilishi wa Kikundi cha wana "Bukoba moja Dira Moja"Ndg Essau Lusabara

Bukoba Club Hotel

Muda: 30:30 – 6:30

HOTUBA KAMILI
... Na Essau Lusabara & Marius Ndyanabo - Wanzilishi
Kwanza kabisa tunapenda kuwapongeza kwa mwitikio wenu, tunajua mlikuwa na shughuli zenu lakini kwa uthamini wenu juu ya tukio hili la kihistoria mmeamua kuhudhuria. Kwa hilo tunawapongeza sana.

Pili, tunapenda tutumie fursa hii kuwashukuru wale wote waliotoa ushirikiano wa ki-hali, kimawazo, kukemea pale wabaya wetu walipotaka kututenganisha, na mengineyo mengi…nao pia tunapenda kuwashukuru sana.

Tukio hili kama yalivyo matukio mengine mengi ya kihistoria, lilianza kama wazo tu. Ni baada ya kukutana watu wawili tukishirikishana habari ya kufanikiwa kwetu sisi lakini pia wanajamii wote - ni kwa nini watu fulani wamefanikwa na wengine tumeendelea kubaki nyuma. Baadhi ya majibu tuliyoibuka nayo ni kama mtakavyo yasikia hapo baadaye…

Huu hatukupenda uwe mwisho, bali mwanzo wa kuyapokea mawazo yenu pia. Kama zilivyotangulia shukrani zetu, shukrani zaidi tungependa ziwaendee Ndg Charles Nyangaya, Mzee Christopher Karurama, Dada Febronia Shumbusho, Ndg Flavius Rwelamira, Ddg Ashiraf, Ndg Erick Kayungi (Singida), Ndg Erick (Dar), Mama Vicktoria, DadaTeddy Methy , Joy Evance (USA) na wengine wengi waliotoa maoni yao kupitia njia zote, kupitia mtandao (Facebook Group Account), kupitia simu na hata kuonana uso kwa uso. Mawazo yenu tumeyachukua na tunayafanyia kazi.

Na wengine hapa mnaombwa kuwasilisha mawazo yenu pia.

Lakini wakati tunajaribu kuchukua maoni ya watu, wengi wamekuwa wakiuliza, ‘Hivi msukumo wenu wa kuanzisha hili ni upi?

Haya yamekuwa majibu yetu:

“Bukoba tumekuwa nyuma sana katika kipindi hiki kuwahi kushuhudiwa katika historia. Na si mtu mmoja mmoja, shujaa, mtawala wala jemedari ndiye anayeunda historia, bali hasa ni mataifa mazima mazima, umma mkubwa wa wananchi wafanyao kazi wenye kuunda thamani za vifaa ndio walio chanzo cha ustaalabu na utamaduni wote.

Yapasa itiliwe mkazo hapa kwamba ‘Si fahamu yetu ndiyo inayoamua kuwako kwetu, bali kuwako kwetu kijamii ndiko kunakoamua fahamu yetu.’ Maendeleo ya kisiasa, kisheria, kifalsafa, kidini, kisanaa, na mengineyo tuanayoyaona yametegemezwa juu ya maendeleo ya kiuchumi. Lakini yote haya huathiriana na pia kuathiri msingi wa kiuchumi. Yatupasa mtu asifikiri kwamba hali ya kiuchumi ndiyo sababu, na ndiyo pekee yenye kutenda, ilhali yote mengine yaliyosalia yana taathira ya kutendwa. Kinyume chake, uathiriano unatukia juu ya msingi wa haja ya kiuchumi, ambayo hatimaye siku zote hujifagilia njia yenyewe.

Sisi ndio waundaji wa historia yetu wenyewe. Wakati wa kuendesha shughuli zetu huyageuza maumbile, jamii na hata nafsi zetu. Tunaunda na kuzalisha thamani zote za mali, za akili na za utamaduni na, kwa mapambano yetu ya kimapinduzi, tunayakomesha mahusiano ya kijamii yaliyokwisha zake na kuweka badala yake, yale yaliyo mapya na ya kimaendeleo zaidi.”

Ni kutokana na ukweli huu, yatupasa kuwa na JAMII moja...jamii ya wana-One Bukoba One Destiny.

Jamii ya wana One Bukoba One Destiny ni ipi? Ni jamii ya watu walio huru walioungana pamoja katika UMOJA au jumuiya yenye kujiendesha yenyewe. Jamii yenye kutengeneza uzalishaji mali na matumizi juu ya msingi wa kisayansi, yenye kudhibiti uchumi kwa kutumia maarifa yake ya kawaida za kiuchumi, na kupanga maendeleo yake ya kudhamiria kwa manufaa ya wote.

Jamii ya wana-One Bukoba One Destiny ni mchupo wa binadamu kutoka ulimwengu wa haja kwendea ulimwengu wa uhuru. Inakusudiwa nini kwa maneno haya “Ulimwengu Wa Uhuru”? Yamaanisha, kwanza, kwamba watu wataendeleza kwa ufahamu timamu na kwa kudhamiria uzalishaji mali kwa manufaa ya watu wote wa jamii na, pili, yamaanisha pia kwamba mtu mara ya kwanza anakuwa ndiye bwana halisi, mwenye fahamu timamu wa maumbile…

One Bukoba One Destiny ndicho KIUNGO chenye kuunganisha nadharia na matendo, falsafa na maisha. Kwa maneno mengine, One Bukoba One Destiny tunatakiwa kutekeleza kwa matendo mawazo ya jamii iliyo huru kutokana na unyonyaji.

Kwa kuthibisha katika makala hii ya ufunguzi kwamba UKOMBOZI wa Bukoba hauwezi kupatikana bila ya ukomeshwaji wa “kila aina ya utumwa”, na tabaka la wanyonge ndilo hasa lenye haki chache zaidi na kukandamizwa zaidi. Wana One Bukoba One Destiny hatuwezi kujikomboa nafsi yetu pasina kuzikomboa sehemu zote nyingine za jamii.

Bali, tunahitaji kujenga jamii ya ubindamu halisi na uliokamilika ambayo yawapatia watu wake wote fursa ya kujiendeleza kwa pande zote. Kwa hivyo, One Bukoba One Destiny tumepiga hatua muhimu ya kwenda mbele; tumepata mwito barabara wa mapambano ya kutimiza ndoto zetu na pia nguvu halisi yenye uwezo wa kuyatekeleza malengo haya.

Lakini pia, jukumu letu ni kuwa na ubora wa kuweza kuelewa hali, mwelekeo na matokeo ya kijumla na hatimaye ya harakati za kuondosha umaskini miongoni mwetu na jamii kwa ujumla. Hivyo yatupasa kuwa na shabaha moja ya kiutu ambayo ni uundaji wa jamii amabayo ndani yake “maendeleo huru ya kila mmoja ni sharti la kupatikana maendeleo huru ya wote.” Ni hapo tu ndipo jamii hii itakapoweza kuandika kwenye beramu yake: Kutoka kwa kila mmoja kwa mujibu wa uwezo wake, kumpa kila mmoja kwa mujibu wa mahitaji yake.

“Tuko Hapa, Bukoba Moja Dira Moja”

Tunawashukuru sana kwa kusikiliza na Mungu Wangu awabariki sana
Next Post Previous Post
Bukobawadau