Bukobawadau

WINFRIDA WILFRED MLEMAVU ZAIDI YA MIAKA 33 SASA APATA UWEZEKANO WA KUTEMBEA:alipata ulemavu akiwa na umri wa Miaka 3,Inasikitisha wapo Wanaume waliomfanyia Unyama na kumpa Mimba,Hanaitaji msaada wa hali na Mali,Jitiada za Mzee Raza wa Izaas Medical Project zamfanya atoe Machozi kwa kutokuamini kile alicho ambiwa......!!!

Winfrida Wilfred pichani ni mwanamke mwenye umri wa Miaka 33ambaye akuweza kuyaamini masikio yake baada ya kuambiwa anaweza akatembea baada ya kuonana na Daktari bingwa wa Mifupa Ndg Wemdelim Shaffer kutoka Taho lake USA.
Miguu ya mlemavu ilionekana hivi na kinacho sikitisha wapo wanaume waliodhubutu kumchezea na kumpatia Ujauzito katika hali hii,na kwa hivi sasa anaye anaye mtoto mwenye umri wa miezi 10 na asiye julikana ni nani Baba yake

Hali hii inasikitisha,inauma na inatia simanzi na inaboa kwa kiasi kikubwa
Bukobawadau tunawaomba Wanaume wenye tabia za kinyama waweza kujilekebisha.

Camera yetu ilishuhudia Bi Winfrida Wilfred akitoa tabasama baada ya kuambiwa anaingia kwenye Chumba cha Upasuaji na baada ya mda alitoa machozi kutoka na hisia zilizo mpata.
Hii ni atua ya mwanzo.
Madaktari na Manesi wakipeana ushirikiano wa hali ya juu.
Hapa ni baada ya Upasuaji na kunyoosha miguu ya Bi Winfrida iliyokuwa imepinda hapo awali.
Wadau picha za tukio hili nyingi zinatisha hivyo hatutaweza kufatanisha kwa kila hatua ilivyokuwa ikiendelea.

Damu nyingi imemtoka na kulazimika kumwekea nyingine
Daktari Wendelim Shaffer akifatilia mapigo ya moyo ya Mgonjwa huyu.
Bi Winfreda Wilfred alipata ulemavu akiwa na umri wa miaka mitatu
Hana msaada wowote pamoja na hali alionayo
Mpaka hivi sasa yupo nyumbani kwa Mzee Raza Fazal maarufu kama BGT.
Mgonjwa huyu anaendelea kusaidia na Bi Edwera msaidizi wa Mzee Raza
Wadau tumejaribu kuweka tukio hili kuonyesha hali ya kuitaji msaada inavyo takiwa kwa watu wengi akiwemo Bi Winfrida
Mdau unaweza kupeleka msaada wako pale Nyumbani kwa Mzee Raza
Au kuwasiliana naye kupitia Maelezo ya habari inayo fuata hapo chini.
Next Post Previous Post
Bukobawadau