Bukobawadau

KONGAMANO LA MAENDELEO MKOANI KAGERA-Mikakati yafanyika,wadau watoa sababu ikiwemo ukilitimba waSerikali,Maadhimio 15 yazingatiwa,Askofu Kilaini,Kanali Masawe watoa Cheche!!!!!!!

Baba Askofu Kilaini akitoa hotuba fupi juu ya sababu ya Mkoa wa Kagera kushuka kimaendeleo hadi kufikia mkoa wa 19 nchini Tanzania.
Juu ya maendeleo amesema kuna haja kubwa ya kushirikisha mihimili mitatu mikubwa katika kufikisha huduma za jamii,maelewano na maendeleo akitaja Serikali kwa kukumbuka halmashauri kama ya Rwamishenye ,Pili vyama vya Ushirika kama BCU sasa ni KCU juu ya mfuko wa Elimu kitu ambacho ndio msingi mkubwa,tatu ni mashirika ya kidini.

Pia Baba Askofu amegusia hali ya umoja mshikamo baina ya wana kagera na katika hilo akawakumbuka watu maarufu watatu akiwemo Marehemu Sheikh Mikidad wa Bakwata,Askofu Kibila wa kilutheli na Cardinal Rugambwa na kusema walifungamana na kushirikiana kwa kila kitu asa katika maamuzi.

BUKOBAWADAU TUNAOMBA WADAU KUPITIA VIDEO HAPO JUU ILI UPATE KUSIKIA MANENO YA ASKOFU NA WADAU WENGINE:nukuu ya leo maendeleo ya Kagera yalitokana na mihimili mitatu kabla ya Uhuru na baada ya Uhuru yaani Serikali,Vyama vya Ushirika na Mashirika ya kidini

Kulia ni Baba Askofu msaidizi jimbo Katoriki la Bukoba Methodius Kilaini
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Kagera Sheikh Mussa Athuman Kagimbo (mkazi wa Nshamba Muleba)
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh Kanali Mstaafu Fabian .I.Masawe
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mh Samwel Kamote
Akiongea na wadau waliojitokeza kwenye Kongamano hilo Mh Masawe amesema huwezi kukuta watu wa Bukoba wamekusanyika na kupanga mambo ya kimaendeleo,mara nyiki uwakuta watu kwenye viwanja vya bukoba club wakichangia vikaonvyav harusi na tafrija mbalimbali kitu ambacho ni tatizo na sio swala endelevu

Pia Mh.Masawe amehoji ni kwa nini watu wasichange pesa ili mgonjwa aliyepo hospitali aweze kupana?!! au kwa nini watu wasichange pesa kwa ajiri ya kumpeleka shule mwanafunzi asiye na uwezo?!!!

Bukobawadau hii tumeipenda
.
Mkuu wa Mkoa Mh.Kanali Masawe picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya Mh.Samwel Kamote.
Mdau Juma Mokili akifanya Majumuisho ya hoja mbalimbali
Mdau akitoa hoja
Mama Lwakatare
Kwahisia kali mdau akibabadua mambo
Wadau pichani wameonyesha kuchomwa na hotuba ya Mkuu wa Mkoa.
Ndg Mdau waweza pia kuona video hiyo kupitia account yetu ya you tube au waweza kuplay hapo juu kama compyuta yako ina suport,hii ni muhimu sana.

Swala la maendeleo halina Umri
Sehemu ya wadau waliojitokeza kwenye kongamano.
Hoja ya kuwaomba wadau waliopo nje ya Nchi kuwekeza Nyumbani kwao imepewa kipaumbele sana
Mdau Abdmalik Tibabimale yeye anasema juu Urasmu wa Watumishi serikalini ni tatizo kubwa na kikwazo cha maendeleo
Wadau wakifatilia kwa umakini
Hii ni kwa ufupi tu ilivyokua Kongamano la Maendeleo ya Kagera baada ya miaka 50 ya Uhuru
hivi punde tu tunakupa moja kwa moja video zinazo onyesha matukio ya watu mbalimbali na kile wanacho kisema
Next Post Previous Post
Bukobawadau