ASEMAVYO MDAU ELEWA SABUNI KUHUSU USAFIRI WA MAITI;Hii ni kutokana na habari tuliotoa kupitia wadau wiki iliopita.
MWANZO HII NI EMAIL TULIOPOKEA KUTOKA KWA MDAU ELEWA SABUNI KUTOKA KYAKA:
elewa sabuni elewa2009@gmail.com
3:32 PM (1 hours ago)
to me. Hello Bukobawadau,
kweli nimesikitika sana kuona hali ya kwetu Bukoba bado tuko nyuma mpaka maiti inabebwa kwa pikipiki yaani thamani ya utu inaishia hapo kweli nimesikitika sana. Sasa tufanyeje kwa waliombali na Bukoba na walioko Bukoba wenyewe tunatakiwa kujikomboa kununua vifaa viwasaidie ndugu zetu walioko vijijini nakumbuka zamani kama unatoka Kyaka pale mlima katoma lazima ukutana na watu wamebeba maiti kwenye baiskeli wanapelekwa vijini kila mtu anaona sioni wakati wa sasa jamani.
Nakumbuka kuna kampuni moja iko Dar es Salaam wanazo Bajaji nzuri zinaweza kubeba maiti, wagonjwa, wamama wajawazito tukiamua tunaweza kufanya harambee kwa ajili ya watu wa Bukoba tukanunua hizo bajiji kama tano tukapeleka kwenye kata ili mwanakijiji anapopatwa na shida kama hii anakodi kijijini na inasaidia hata kwa maendeleo. Kuna kijiji kimoja mtwara wanakijini baada ya kupata shida walichanga wanakijiji wakainunu kwa 10,000,000/= inawasaidia sana na kijiji ndo kilichagua mtu atakayeindesha na kuitengeneza yaani wako sembuse sisi watu kutoka Bk tunashindwa nini?
hizi Bajaji zina uwezo wa kubeba Mgonjwa, muuguzi na msaidizi wa mgonjwa zina saidia sana naomba wahaya tukae tulitafakali kwa kina tuwe kama wenzetu wachaga make wao usafiri umejaa vijijini sio kama sisi. nakutumia na picha za bajaj tunaweza kuandaa harambee ya siku moja tukapata hela kibao tukawasaidia wenzetu wa vijijini. hii kampuni iko Dar
mdau toka kyaka
Pikipiki ikiwa mwendo wa kasi inakoa Ndolage Hosp.kuelekea Ichwandimi kupitia Nyakigando maeneo ya Rubale.
Mfano wa bajaji za kubebea wagonjwa