Bukobawadau

BUKOBAWADAU TUMESIKITISHWA NA KIFO CHA NDG BEATUS KAGASHE KILICHOTOKEA USIKU WA KUAMKIA JANA

Marehemu Beatus Kagashe. Bukobawadau blogspot tumesikitishwa na kifo cha mwanahabari mwenzetu Beatus Kagashe kilitokea usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya Ocean Road, Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa Bukobawadau blogspot tunatoa pole kwa Wazazi wa marehemu Bwana na Bi Deo Kagashe,


Wadogo zake marehemu Katunzi Kagashe na George Kagashe pia Kaka wa marehemu Denis Kagashe,wanafunzi wenzake wa Ihungo na Mpwapwa na wafanyakazi wenzake wa Mwananchi communication Limited(MCL) Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Amen.
HISTORIA YA MAREHEMU: Marehemu Beatus Kagashe alizaliwa Februari 23, 1981 mkoani Kagera na alipata elimu ya msingi katika Shule ya Bilele iliyoko Bukoba Mjini kati ya mwaka 1990 na 1996, alijiunga na Shule ya Sekondari Ihungo kuanzia mwaka 1997 mpaka 2000 kabla ya kujiunga na Shule Sekondari Mpwapwa kwa masomo ya kidato cha tano na sita.


 Mwaka 2004, alichaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kusoma kozi ya uandishi wa habari (Bachelor ofn Arts Journalism) katika Taasisi ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (IJMC) alipohitimu mwaka 2007. Alijiunga na masomo ya shahada ya uzamili katika masuala ya utawala (Masters in Public Administration) katika Chuo Kikuu cha Mzumbe mwaka 2010 na kuhitimu Novemba mwaka jana.
Next Post Previous Post
Bukobawadau