Bukobawadau

HAPA NA PALE NA CAMERA YETU BUKOBA HII LEO

Ni maeneo ya stend kuu mjini Bukoba hii leo mpaka sasa haina hadhi ya kuitwa stend kuu

Barabara:Ni jambo la kujivunia kwa wanakagera kwa kuweza kuwa na barabara nzuri na zenye lami kuanzia za kuingia mpaka za mitaani na kwa kiasi kikubwa zikiwa safi
Biashara:Mkoa wa Kagera bado haujafanya vya kutosha katika kuimarisha biashara na kutumia nafasi zilizopo kwa ajiri ya kuwaendeleza wakazi wake,mfano, mpaka leo hapana kituo cha mabasi chenye hadhi ya kuitwa stand ya mabus kwa maana bado stand ni ndogo na bado ni ya matope,Hapa kuna connection ya nchi kama 4 na wasafiri wanakutana pale kwenda Uganda,Rwanda,Burundi na hata Kenya..mkoa unahitaji kuliona hili mapema kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Bukoba mjini na wabunge wa wilaya nyingine.

Bukobawadau japo tulimsikia Mh.Meya Anatory Aman akisema wameanza ujenzi wa stend mpya na ya kisasa itakayo kuwa na hadhi ya kipekee afrika masharika kama tulivyo weza kuwajulisha kupitia blog hii bado changamoto ni kubwa sana asa tukiangalia mipango ilivyo mingi na hali,vyanzo vya mapato na kile kinacho onekana uharaka wa kutaka kuitwa Jiji kufikia 2015

Katika hili tunaomba mawazo yenu wadau kwa kutoa comment za moja kwa moja au kupitia facebook page yetu mwisho kabisa wa page hii.

Hapa ni Q bar iliopo mjini hapa mitaa ya uswahilini Bilele.
Jitiada kubwa za Usafi wa Mji kutoka kwa Mh.Massawe haya ni maeneo yanayo takiwa kufanyiwa kazi na Manispaa hivi ndivyo camera yetu ilivyo angaza barabara ya Arusha.

Mtazamo wangu ni juu ya faini wanazotozwa watu kwa sababu ya usafi wa mazingira zingeambatana na semina elekezi ili kutokomeza kabia tatizo hili (watu waelimishwe)
Next Post Previous Post
Bukobawadau