Bukobawadau

BREAKING NEWZZZZZZ:NI MASAA 20 SASA MKOA MZIMA UPO GIZANI,Tatizo mpaka sasa halijajulikani!!!!Huduma ya maji pia ni kitendawili kutokana na kukosekana kwa Umeme...

Chanzo cha Umeme wa maji Bugonzi Ndolage Kamachumu, Huu ni mfano wa namna tunavyo weza kujipanga na kuepukana na sakata hili la Umeme.

 Ikiwa toka jioni ya jana mpaka sasa hali ya Umeme na Maji ni tete mkoani Kagera hakuna tamko lolote lililo tolewa na Tanesco au Viongozi wa mkoa.

Tetesi mtaani ni kwamba kuna tatizo la kiufundi uko Nchini Uganda tunapotoa Umeme au tunadaiwa deni kubwa na Serikali ya Uganda.

 Bukobawadau tupo katika jitiada za kuwasiliana na wahusika ili tupate kuelewa tatizo ni nini asa.
Next Post Previous Post
Bukobawadau