HII INASIKITISHA SANA TENA SANA NA NI AIBU KISA GARI LA TAKATAKA NI BOVU!!!!
Haaahhh!!!!Nashangazwa na Ghuba la eneo hili ikiwa ni siku ya pili toka tumeliongelea.....
Jioni ya leo imeniladhimu kupitia eneo la Ghuba hili la kuifadhia takataka ni baada ya kupata msg nyingi kwenye simu yangu kuhusiana na kile nilicho kiongelea jana kuhusu uchelewaji wa kuzoa taka.
Msg moja ikitoka kwa mdau wa kitengo cha Mazingira hapa Manispaa AKILAUMA kwamba eneo likiwa safi hatusemi na wala hatuweki picha.
Binafsi nilidhani swala hili wamelishughulikia hivyo ikaniladhimu kufika ili nipate ata picha mbili tatu badala yake nakutana na harufu mbaya ya Uchafu uliolundikana zaidi ya jana.!!