Bukobawadau

NDOLAGE KAMACHUMU HII LEO


Hii ni sehemu moja wapo na maarufu sana kwa wakazi wa Kamachumu, Huu ni Mto(AMSOKE)maji ya hapa yana raha yake sana,tofauti na kasi yanayokuwa nayo kutokea vyanzo vya Mto Nyangorogoro na Izinaizibu bado Maji haya yana sifa ya ubaridi wa kipekee. Bukobawadau tunaomba kwa yeyote anaye jua vyema sehemu hizi na eneo hili atusaidie maelezo ya kina asa ya kihistoria kupitia sehemu ya comment hapo chini.
Mto Izinaizibu,Haya ni Maji ya Chemichemi yenye ubora wa kipekee Nchini Tanzania Nisinge penda kuonekana naongea sana au napigia debe mambo haya ila nimewasikia wakazi wa Kamachumu na Vitongoji vya Jirani wakisema;'haya maji ni ZAMZAM ya Kamachumu'.
Nyumba ya Familia na Chimbuko la Ukoo wa Mpocho hapo Kamachumu
Kijana wa Kiume akielekea Mtoni.
Jengo la hospitali ya Ndolage.
Mdau hapa ni Bugonzi Ndolage Kamachumu kwenye Chanzo cha Umeme wa Maji. Camera yetu ndio imefika eneo hili Tukio kamili litafatia ngoja tufanye mchakato wa kushuka uko bondeni ikiwezekana.
Next Post Previous Post
Bukobawadau