Serikali ya Zimbabwe yaondolewa vikwazo na EU
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe
Muungano wa Ulaya umewaondolea vikwazo baadhi ya
maafisa wakuu wa serikali ya Zimbabwe, ingawa utaendelea kushikilia mali
ya rais wa nchi hiyo Robert Mugabe pamoja na washirika wake wa karibu.
Kwa mujibu wa muungano huo, vikwazo vya usafiri
dhidi ya mawaziri wawili viliondolewa ili kushinikiza serikali
kuharakisha mchakato wa mageuzi.
Lakini msemaji wa chama cha rais Robert
Mugabe,alipinga hatua hiyo akitaja vikwazo hivyo kama vinavyokiuka
sheria, vyenye misingi ya ubaguzi wa rangi na vitakavyoathiri uchumi wa
nchi.
Muungano huo pia uliondoa takriban kampuni
ishirini za serikali kwenye orodha hiyo ambazo muungano huo ulidai kuwa
zilisaidia kufadhili vurugu nchini Zimbabwe.
Ingawa Zimbabwe imepiga hatua katika mchakato wa
kuunda katiba mpya, na kuimarisha uchumi, Muungano huo ungali na
wasiwasi ikiwa ahadi zilizowekwa baada ya uchaguzi uliokumbwa na vurugu
mwaka 2008, ikiwemo ahadi za kufanyia mabadiliko idara ya polisi
hazijaweza