Bukobawadau

WADAU WAUAGA MWILI WA MAREHEMU KURWA KASSIM (NDG PACHA WA MAMA RUBBY)

Mwili wa Marehemu ukitolewa ndani huku umati mkubwa wa watu ukishuhudia tukio hilo 
Gali lililobeba mwili wa Marehemu Kulua likiwa tayari kwa safari ya kuelekea Mjini Tabora nyumbani kwao na  marehemu 
Ndg Hilal Abdul Gade  mpwa wa marehemu akiwa tayari kwa safari
Mdau akimfariji Mfiwa Mama Rubby 
Wafiwa wakiwa tayari kwa safari.
Anaonekana Mama Mkude na Mama Abdul marafiki wakubwa wa familia wakiteta jambo.
Kutoka kushoto ni Ndg E.Nyambo,Peter Mgisha,Said Bunduki, Ndg Matovelo na Moody Salum Mawingo
 Ndg Salum Muhammed Khalfan A-l Suqry akitoa neno kwa niaba ya familia ya wafiwa  wakati wa kuaga mwili wa marehemu Kulua ikiwa unapelekwa nyumbani kwao Tabora
Anaonekana Ndg Ismail Ziaka, Mwalimu King na Ndg Omary Kazinja
Dua ikiongozwa na Sheikh Haruna Kichwabuta
Wadau mbalimbali waliofika Nyumbani kwa Mama Rubby kuhani na  kuaga mwili wa Marehemu Kulua..
Sehemu ya akina mama waliofika msibani
Anaonekana Mama Rubby pichani  kulia  katika hali ya majonzi,simanzi na huzuni mkubwa wa kuondokewa na  ndg yake, kaka yake mpendwa  ambaye ni Pacha mwenzake.
Wadau mbalimbali waliofika kufariji wafiwa.
Msiba huu umetokea ghafla mchana wa leo baada ya marehemu kusumbuliwa na moyo na kukimbizwa hospital ya Mkoa  kwa ajili ya matibabu ambapo alilazwa hadi mauti yanamkuta mchana wa leo.

Bukobawadau tunatoa pole kwa wafiwa

Inna lilah waina ilah lajuun. mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi "Amina

Next Post Previous Post
Bukobawadau