Whitney Houston Elizabeth (9 Agosti 1963 - 11 Februari 2012)
Whitney Houston Elizabeth Mwanamuziki mashuhuri wa Marekani
amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 48.
(9 Agosti 1963 - 11 Februari 2012) alikuwa mwimbaji, mwigizaji, mtayarishaji.
Amefikia mafanikio makubwa sana mfano. Mwaka 2009, Guinness World Records alitangazwa kama mwanamuziki bora wa kike kutokana na tuzo nyingi alizo jipatia kwa wakati wote.
Nimegundua Whitney Houston alikuwa na mashabiki wengi sana duniani kote na hii leo nimepokea simu nyingi kutoka kwa wadau mbalimbali wakiwa na lengo la kunijulisha juu ya kifo cha Mwanamuziki huyu na wengine wakionyesha simanzi na majonzi makubwa juu ya kifo chaWhitney.
Mpaka nafanya Jitiada hizi mie Mc Baraka sijapata Sababu za kifo chake na mahala alipofariki bado hazifahamiki,
Orodha za tuzo mbalimbali Awards Emmy alipata mara 2, Grammy Awards anazo 6 , Billboard Music Awards tuzo 30 , American Music Awards tuzo 22
Whitney Houston ni msanii wa kuchukua mfululizo
No 1 Billboard
Hot 100 hits hapo tunaongelea wimbo wa mapenzi yangu yote ni kwa ajili yako yaani My Love is your love "I Wanna Dance na Somebody Loves Me (mtu flani ananipenda) ,Nyimbo kama Emotional na nyingine nyingi.
Na kama nikibahatika kufanya enterview na wasanii wengi wa kike wa Tanzania na East Afrika kiujumla utawasikia wakisema wanampenda na wanafata nyayo za Whitney hapo namaanisha Juliana Kanyamozi, JayDee, Aman ,Linnah na wengine wengi ,
Whitney Houston mwaka 2010 alikuwa mmoja kati yawasanii wanao ongoza kwa mauzo dunia zaidi ya copy 170 milioni zimeuzwa duniani kote ikiwa ni single mbalimbali ,Album na Video.
,
Whitney HoustonHouston alianza kuimba na New Jersey katika kanisa la injili kama mwana kwaya akiwa na umri wa miaka 11.
Na badae alijiunga na mama yake na kuanza kuimba pamoja katika klabu ya usiku katika eneo la New York City, ndipo alipo pata kujiunga na Arista Records studio ya mtu mmoja mtata sana ajulikanae kama Clive Davis .
Mpaka hivi sasa kazi za Whitney ni sawa na Almasi au Dhahabu ikiwa ni movie alizo cheza,nyimbo zake zote katika album mbalimbali na soundtrack kama tatu zilizotumika.
Bobby Brown na Whtitney Houston
Whitney kama mmoja wa wanamuziki wenye mafanikio
makubwa duniani, na mcheza filamu mbalimbali vile The Bodyguard na Waiting to Exhale.
Fani yake iliwahi kuzongwa na matumizi ya dawa za kulevya na maisha yake yenye matatizo katika ndoa na msanii Bobby Brown kitu kinacho pelekea mpaka hivi sasa wadau wengi wamtazame Bobby Brown kwa jicho la pili nikiwa na maanisha kutia shaka juu ya kuchangia katika mabadiliko ya Maisha ya Whitney.
Bobby Brown aliwahi kusema katika kitabu chake namnukuu;“I never
used cocaine until after I met Whitney. Before then, I had experimented
with other drugs, but marijuana was my drug of choice,” Brown writes in
“Bobby Brown: The Truth, the Whole Truth and Nothing But,” out next
month. “At one point in my life, I used drugs uncontrollably. I was
using everything I could get my hands on, from cocaine to heroin, weed
and cooked cocaine.”