Bukobawadau

AIBU YA MAN U OLD TRAFFORD

Mashabiki wa Manchester United walibaki jana vinywa wazi pale timu yao ilipochapwa mabao matatu kwa mbili na Athletico Bilbao katika uwanja wao wa Old Trafford.
Kocha wa Man U Sir Alex Ferguson.

Timu hiyo ya Uhispania iliizidi maarifa mashetani wekundu katika mchuano wa hatua ya timu 16 bora ya mechi za kombe la ligi ya Euro.
Man U ndio waliokuwa wakwanza kufunga bao katika dakika ya 22 kupitia mwamba wake Wayne Rooney.

 Lakini baada ya hapo Athletico ilianza kuihangaisha ngome ya Manchester United . Na kukiwa kumesalia dakika chache tu kwa timu hizo kwenda mapumziko Fernando Llorente aliisawazishia Athletico Bilbao. Baadae Oscar de Marcos na Iker Muniain wakafanya magoli kuwa 1-3.

Lakini kabla ya kipyenga cha mwisho Rooney aliipatia Man U bao lake la pili kupitia mkwaju wa penalti.
Baada ya mechi hiyo Meneja wa Manchester United akiri kuwa timu yake ilizidiwa maarifa na Athletico Bilbao ya Uhispania.
" Walikuwa wazuri kutushinda . Kwetu itakuwa ni kazi ya kupanda mlima", Ferguson alisema.

Lakini mkufunzi huyo wa Man U bado ni mwingi wa matumaini kwamba wanauwezo wa kifunga Athletico Bilbao watakapowatembelea kwao baada ya wiki mbili.
Next Post Previous Post
Bukobawadau