Bukobawadau

BREAKING NEWWWZZ!!!! UCHAGUZI WA KRFA UMEISHA KWA AMANI NA Ndg JAMAL MALINZI NA KAMBI YAKE WAIBUKA KIDEDEA

 Mwenyekiti mpya wa KRFA Ndg Jamal Malinzi aliyejipatia kura 22 kati ya 24 zilizopigwa.hapa ilikuwa kipindi anatoa maelezo yake kuwa atawafanyia nini wana Kagera iwapo watampa ushindi,sasa ameshinda wadau tnasubiri kwa hamu utekelezaji wa ahadi za washindi wote
 Ndg Falidh Al-qusaib aliyekuwa anawania nafasi ya uenyekiti na Ndg Malinzi,ila hakuweza kuzifanya kura zitoshe,ila ni mwanamichezo wa kweli pia wa siku nyingi na mchango wake una heshimika
 Katibu wa kamati ya uchaguzi ya KRFA mama Meddy akiingia na masanduku ya kupigia kura muda mfupi kabla ya kazi hiyo kuanza.
 Katibu makini akitoa maelezo ni namna gani zoezi la kuchagua viongozi litakavyofanyika,umakini wa mama huyu umesababisha uchaguzi kuwa huru na haki bila malalamiko yoyote.
 Wajumbe wakiendela na upigaji kura,hapa anaonekana mtalaamu wa wataalamu Ndg Geofrey wa Muleba akitimiza haki yake ya kupiga kura


 Katibu mkuu mpya Mpambanaji Salumu Umande Chama akipongezwa na wadau,anaonekana Afisa utamaduni na kaka Mkubwa na Nyuma mgeni Rasmi Afisa michezo,hii ni baada ya kikao kwisha
Mdau Hamimu Mahmudu Kangezi furaha yake ipo wazi kabisa,anaonekana akimpongeza kwa bashasha mwenyekiti mpya Ndg Jamal Malinzi


Hawa ndio washindi na hizo ni picha zao za pamoja wakiwa na nyuso za furaha kupita maelezo,hapo pia yupo mjumbe mteuliwa Ndg kiiza wa pili kulia aliyeteuliwa na na Swahiba wake mkuu Mwenyekiti Jamal Malizi muda Mfupi baada ya kutangazwa mshindi
 Didas Zimbihile ni mwenye furaha akipongezana na wenzie baada ya ushindi
 TFF kama ilivyo ada ilituma wajumbe wawili kuja kusimamia uchaguzi huu,mwenye miwani hapo ni miongoni mwao
Mdau Jamal Kalumuna akiwa na katibu Mpya,pembeni Ndg Ruge Masabala na Mr White wa kashai na mbishi Abdul razak wa Kasibante radio wakitoka ukumbini
 Ni vigumu sana kuamini yaliyotokea hasa kwa wadau hawa,aliyetupa mgogo na tshirt kama nyekundu ni kijana Abdul al maarufu Abdu Bonge na kaka yake kwa mbele Bwana Musa,camera man wetu na mweka hazina mpya mwenye shati ya draft
 Mbishi huyu uwa ana pilika ile mbaya kwenye matukio,sijui furaha yake inatokea wapi,wacha tumpongeze
Mzee Sadick Galiatano,sijui alikuwa upande gani ila kura au mapenzi ni siri ya mtu,maana katika uchaguzi huu tumeshuhudia watu wakipata kura 0,na wengine kura 1,hii ni kukomaa kwa demokrasia na sisi kama BUKOBAWADAU tunasema asiyekubali kushindwa si.................tujipange kusukuma soka letu wote mbele.



Next Post Previous Post
Bukobawadau