Bukobawadau

HAPA NA PALE NA CAMERA YETU;Wasanii wa THT wawasili mjini hapa ni katika Kampaini ya ZINDUKA!!!!!

 KUNDI la Tanzania House of Talent (THT), limewasili mjini hapa  jana,kundi hili lipo katika  ziara  ya kuelimisha wananchi kuhusu ugonjwa wa malaria.

Ziara hiyo inahusisha mikoa  mingine ya kanda ya ziwa,ambapo wasanii hao watafika vijijini kuelimisha wanafunzi na jamii kwa ujumla kuhusu ugonjwa huo kupitia sanaa.

Akizungumza na Bukobawadau  blog mmoja wa viongozi wa kundi hili  Ndg Muhdini ambae pia ni dreva wa gari lao; Alisema wasanii hao watatumia sanaa ya maigizo, nyimbo za kawaida na zile za asili kufikisha ujumbe kwa jamii.

Pia Ndg Muhdini akasema tayari wamemaliza ziara wilayani Karagwe,na wapo mjini hapa kwa mapumziko ya siku moja kabla ya kuelekea Wilayani Misenyi. 
** Pichani anaonekana  mtoza KODI wa Manispaa akitaka ushuru wa parking**
Sanaa inafanikisha kuelimisha jamii juu ya maambukizi ya malaria na namna ya kujikinga na marelia.
Next Post Previous Post
Bukobawadau