MSIMAMO WA LIGI KUU ENGLAND;Manchester United Kileleni.
Manchester United imefanikiwa
kukalia kiti cha Ligi ya Kuu ya England kwa mabao mawili yaliyopachikwa
na Wayne Rooney na kuilaza West Brom.
Rooney aliifungia Manchester United bao la
kwanza kabla ya mapumziko, alipounganisha mpira uliopigwa na Javier
Hernandez ambao ulimpita mlinda mlango Ben Foster.
Mshambuliaji huyo wa Manchester United alifunga
tena bao la pili kwa mkwaju wa penalti, wakati mlinzi wa West Brom Jonas
Olsson alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuoneshwa kadi ya pili
ya njano.
Wakiwa wamesaliwa na michezo 10 kabla ya msimu
wa ligi kumalizika, Manchester United sasa wanapewa nafasi nzuri ya
kutetea ubingwa wake baada ya Manchester City kuteleza.
Matumaini ya Manchester City kunyakua ubingwa wa
Ligi Kuu ya Kandanda ya England yaliingia dosari baada ya bao la kichwa
dakika za mwisho la Luke Moore lilipoipatia Swansea ushindi wa bao 1-0.
Swansea City kwa ushindi huo sasa imeacha wazi
mbio za kuwania ubingwa ligi ya England baada ya ushindi huo katika
uwanja wao wa Liberty.
Kikosi cha Roberto Mancini kiliponea chupuchupu
kufungwa dakika za mwanzo za mchezo wakati Joe Hart alipookoa mkwaju wa
penalti wa Scott Sinclair baada ya Hart kumuangusha Wayne Routledge
ndani ya sanduku la hatari.
Swansea ilipata bao lake hilo moja baada ya
Moore kuunganisha kwa kichwa mpira wa pembeni wa Routledge zikiwa
zimesalia dakika saba kabla mchezo kumalizika.
City hawakucheza vizuri ingawa Micah Richards dakika za mwisho alifunga bao ambalo lilikataliwa kwa vile alikuwa ameotea.
Manchester City sasa wanashikilia nafasi ya pili wakiwa na pointi 66 na Manchester United wamekusanya pointi 67.
chanzo cha habari ni BBC