Bukobawadau

MTOTO WA DADA SALOME aka Chui na London APATA UBATIZO

 Hapo anaonekana baba wa ubatizo mtumishi wa mungu kaka mkubwa akiwa na kijana AIVAN TUMAINI ALMACHIUS KILAJA katika hatua za kuelekea kwenye kukamilisha tukio la UBATIZO.
 Kwa mafuta haya unabatizwa kijana AIVIAN TUMAINI
Kwa msalaba huu unabatizwa na ufate utumishi katika dini hii kama alivyo baba yako wa ubatizo.
 Kwa kitambaa hiki cheupe ninakupa moyo safi mweupe usio na doa katika mambo yote matakatifu humu duniani.
 Mama na mwana,anaonekana mama mzazi wa AIVAN bi Salome akiwa na Mwanae Kanisani kwa raha zaoooo.
Kamanda mwenyewe akiwa kwenye pozi zito baada ya kupokea sakramenti ya UBATIZO 
 Hakika wamependeza sana mama na mtoto wake sio mchezo,sisi Bukobawadau tumekubali
 Kijana akiwa na Mjomba wake pia na Bibi yake katika pozi nje ya kanisa.
Baada ya kumaliza ya kanisani,Bibi mtu alitumia muda huu kuwakaribisha wageni wao kwenye sherehe kamambe ya kukata na shoka ndani ya ukumbi wa hotel ya COFFEE TREE INN kuja kusherehekea na kijana wao huku wakipata vitu.

BUKOBAWADAU TUNAMPONGEZA DADA YETU SALOME KWA KUFANIKISHA ILI,PIA TUNAMTAKIA UTUMISHI BORA WA KIROHO NA KI IMANI KIJANA AIVAN TUMAINI KILAJA.....NA MUNGU AMPE AFYA NJEMA NA MAISHA MAREFU
Next Post Previous Post
Bukobawadau