Bukobawadau

USHINDI WA JANA WA MAN U;ferguson asema Valencia ana mchango Mkubwa!!!

 Winga machachali alie changia kwa kiasi kikubwa ushindi wa bao 1-0 zidi ya Fulhamu

Bao hilo lilifungwa katika dakika ya 29 ya kipindi cha kwanza pale Rooney alipopokea pasi safi kutoka kwa Jonny Evans.

Kwa ushindi huo sasa Mashetani wekundi wameipiku Man City kwa alama tatu.
Kufikia sasa timu zote zimecheza mechi 30 kila mmoja.
 Wayne Rooney baada yakuipatia Man U bao la ushindi.

 Manchester City sasa wanakibarua kigumu cha kuziba pengo la alama tatu kwani siku ya jumamosi tarehe 31 wataikaribisha Sunderland.

Vijana hao wa Roberto Mancini itawabidi waombe sana Man U wapoteze mechi yao ya siku ya Jumatatu ijayo tarehe 2 April watakapo watembelea Blackburn.

Hata hivyo mkufunzi wa Fulham Martin Jol amelalama kuwa walinyimwa mkwaju wa penalti.
Hii ni baada da ya Michael Carrick wa Manchester United kuonekana kumuangusha mshambulizi Danny Murphy katika eneo la hatari katika dakika ya 87.
meneja huyo wa Fulham amenukulikwa akisema kuwa kila mtu aliyeshuhudia mechi hiyo alitarajia wapewe penati.
Next Post Previous Post
Bukobawadau