BABA WA 'LULU' AZUNGUMZA NA MICHUZI BLOG
Michael Edward Kimemeta
Michael Edward Kimemeta (49) mzaliwa wa Rombo, Kilimanjaro, baba mzazi wa Elizabeth Michael "Lulu" anayehusishwa na kifo cha marehemu Steven Charles Kanumba, akizungumza na Dixon Busagaga wa "Globu ya Jamii" leo huko Moshi, amesema alimtambua Steven Kanumba kama mwalimu wa mwanaye na kustishwa na taarifa za kuwa walikuwa wapenzi.
Zifuatazo ni nukuu za taarifa hiyo:
“Hatukutegemea kama Marehemu Kanumba angeweza kuwa na mahusiano y kimapenzi na binti yetu; kwanza ndiye tuliyekuwa tukimtegemea kwa kiasi kikubwa katika kuendeleza na kukikuza kipaji alichokuwa nacho Elizabeth”, alisema baba mtu.
“Ninaomba Wanasheria na wanaharakati wa haki za kibinadamu kuingilia suala hili na kusaidia katika kupatikana kwa haki dhidi ya shtaka la mauaji linalomkabili binti yangu Elizabeth na pia naomba swala hili lisichukuliwe kishabiki ama kwa hisia bali haki ichukue mkondo wake”alisema.
“Ushiriki wa mwanangu kuhusu mambo ya sanaa nilikwishapata wasiwasi na mama yake mzazi alikuwa akiwasiliana na Marehemu Kanumba enzi za uihai wake ambaye alikuwa anamhakikishia usalama wa Lulu na kusema kuwa ataendele kubaki kama mwalimu… lakini leo nasikia alikuwa ni mpenzi - nilishtushwa” alisema Kimemeta.
Amesikitishwa kwa kutokuhudhuria shughuli za maziko kwa kuhofia usalama wake, na kusema hali itakaporuhusu hatasita kufika nyumbani kwa marehemu kutoa pole.
Soma habari kamili kwenye "Globu ya Jamii" (credits: IssaMichuzi.blogspot.com)