BARCELONA YAFUDHU ROBO FAINALI BAADA YA KUIFUNGA 3-1 AC MILAN;Lione Messi avunja rekodi ya Mabao katika msimu mmoja wa Ligi ya Mabingwa.
Mabao mawili ya Lione Messi yaliopatikana dakika 11 na 41 kwa njia ya penati yamemfanya kuandika rekodi ya pekee kwa kufunga jumla ya mabao 14 katika msimu mmoja wa ligi ya Mabingwa.
Bao la 3 la Barcelona limepatikana mnamo dakika ya 53 kupitia kwa Andres Iniesta Lujan kwa matokeo hayo Barcelona imefudhu robo fainal kwa (agg 3-1) mechi ya kwanza timu hizi zilitoka sare ya 0-0.
Barcelona wameutimia vyema uwanja wao wa Nyumbani Camp Nou watakutana na Mshindi kati ya Chelsea na Benfica.