BREAKING NEWZZZZ;Katibu wa Kamati ya Wabunge wa Chama cha Mapinduzi, Jenista Mhagama, azungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma mara baada ya kumalizika kwa kikao ambacho kimewashauri mawaziri wanane kujiuzulu.Tarifa kamili itafata kadili tutakavyo pata habari.
Wanaotakiwa kuondoka ni Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu, Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),George Mkuchika, Waziri wa Kilimo Chakula na Ushurika Jumanne Maghembe na Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda.
Hata hivyo, baadhi ya Mawaziri hao, wameelezea kuwa wataandika barua kwa Rais Kikwete kuelezea uozo wote uliosababisha kusakamwa kwao, baadhi wakidai kwamba hawahusiki kwa lolote na mambo wanayotuhumiwa nayo, huku baadhi wakiona mambo ni mazito na kuamua kujiondoa usiku huu.
Habari kwa hisani ya Mtandao wa Fikra Pevu