HAPA NA PALE NA CAMERA YETU VIUNGA VYA MJINI HAPA HII LEO.
Maeneo ya Uwanja wa Uhuru hali mchana wa leo hali ni shwari kama inavyo onekana.
Mwonekano wa Jengo jipya la Chama cha Walimu Mkoa wa Kagera lililopo mitaa ya Uswahilini(Bilele)na kwa mbali ni maeneo ya Mlimani Kibeta.
Katika pitapita nakutana na Mdau Ruge akijipatia Msosi wa mchana katika Mghahawa wa Manyema.
Barabara ya Tupendane shughuli za hapa na pale zikiendelea mchana wa leo.
Barabara ya Kashozi maeneo ya Kanisa la KKKT.
Makutano ya barabara ya Kashozi ,barabara Tupendane na barabara ya Jamhuri kwa ufupi ni kwamba mji umetulia hakuna hekaheka ipasavyo.
Bango la tangazo juu ya Ujio wa Msanii wa Hip hop Roma Mkatoliki tarehe 8.4.2012 siku ya Pasaka.
Onyesho limedhaminiwa na Tang Records.
Napita maeneo ya ITL nakuta jamaa wanashusha vitu mbalimbali vya mitumba ni Mali ya Mdau Twalib, ukipenda waweza kufika kuona bidhaa zao na kujipatia mahitaji