KIMENUKA BUNGENI ZITTO AMTAKA WAZIRI MKUU KUJIUZULU!!!!
Mh. Zitto Kabwe.
Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Mh Zitto Kabwe amelitaarifu Bunge kuwa mchakato unaandaliwa kukusanya saini za wabunge 70 ili kuweza kupeleka hoja ya kulitaka Bunge kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.
Zitto amesema zoezi zima la saini hizo linaanza kesho asubuhi Mlangoni ili kabla ya Jumatatu liwe limekamilika ili kuweza kuwasilisha hoja hiyo ili Wabunge na Bunge limshinikize Waziri mkuu kujiuzulu au vinginevyo mawaziri wote waliotajwa kuhusika na ubadhirifu wa fedha za umma katika ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wawe wamejiuzulu badala yake.
Hii imetokea jioni hii Bungeni Dodoma ambapo wabunge wengi bila kujali itikadi za vyama vyao wameonekana kukerwa na utendaji mbovu wa mawaziri wa Serikali ya JK.