Bukobawadau

MADAKTARI WAELEZA KILICHOMUUA KANUMBA

Msanii nyota wa filamu nchini, Steven Kanumba amefariki kutokana na tatizo la mtikisiko wa ubongo linalojulikana kitaalamu kama BRAIN CONCUSSION, taarifa za kitabibu zimeeleza.

 Taarifa hizo za ndani, zimepatikana jana baada ya jopo la madaktari bingwa watano wa hospitali ya taifa Muhimbili kuufanyia uchunguzi mwili wa marehem, zimeeleza kuwa tatizo hilo linaweza kumfanya mtu apoteze maisha mara moja au baada ya siku kadhaa.Mmoja wa madaktari hao ambae aliomba jina lake lisitajwe gazetini alisema waligundua tatizo hilo baada ya kumfanyia uchunguzi huo kwa zaidi ya masaa mawili.

"tulianza kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 6:45 mchana na tukagundua kuwa marehemu alifariki kutokana na mtikisiko wa ubongo kwa kitaalamu Brain Concussion" alisema.
 Kanumba alipata mtikisko huo ambao husababisha kufeli kwa mfumo wa upumuaji (cardio-respiratory failure) "kilichomuua hasa ni mtikisiko wa ubongo, ambao endapo unatokea katika sehem ya nyuma ua ubongo (cerebram), huua kwa haraka" alisema daktari huyo na kuongeza kuwa mtikisiko wa ubongo wa nyuma husababusha matatizo ya mfumo wa upumuaji na hilo limeonekana katika mwili wake.

"Baada ya ubongo wake kutikiswa kwa nguvu, mfumo wa upumuaji unafeli na ndio maana tumekuta kucha za kanumba zikiwa na rangi ya blue, huku mapafu yake yakiwa yamevilia damu na kubadilika kuwa kama maini, hizo ni dalili za kufeli kwa mfumo wa upumuaji"

 "Mtu aliepata mtikisko wa ubongo huweza kutokwa na mapovu mdomoni na hukoroma kabla ya kukata roho na ndivyo ilivyokuwa kwa Kanumba kabla hajafariki.

 Daktari mwingine alieshiriki katika uchunguzi huo ambae pia aliomba jina lake lisitahwe alisema ubongo wa mwigizaji huyo umevimba na kushuka karibu na uti wa mgongo na hivyo kuathiri mfumo wa upumuaji. Alisema sehemu ya maini na maji maji ya machoni ya marehemu, vimepelekwa kwa mkemia mkuu wa Serikali ili kubaini endapo kuna sumu au kitu kingine katika mwili huo.
Next Post Previous Post
Bukobawadau