WADAU WAUSINDIKIZA MFUNGO WA KWARESMA KWA KUTOA SADAKA KATIKA KITUO CHA WAZEE KILICHOPO KILIMA,BUGABO.
wwwwWadau hawa wamejiuliza hivi ni kwanini tusishiriki shangwe na hawa wazee wetu wa kituo cha.....kilichopo.... maalumu kwa kuwatunza wazee wasio na uwezo,walemavu,vipofu,viziwi na watoto yatima kwa kula,kunywa nao ikiwa ni sehemu ya Pasaka yao?
Bi SalomeMdada salome aka Chui na London akimnawisha maji kabla ya kula mwana kituo,ikiwa ni ishara ya upendo na msaada kwa mzee huyo
kakaKaka mkuu akipakuwa na kuhudumia wazee chakula
bibi huyu mcheshi kabisa mwenye ulemavu wa macho ila anao ufahamu mkubwa akikonga pilau ndizi huku akisukumia na Kitu RWENZORI
Zoezi la kuwanawisha Wazee lilikuwa la wote kuonesha upendo anaonekana Hope Makoko na Mdau Optaty Henry(katibu)wakiwajibika.
Mahakuli yenyewe kutoka Bukoba Mjini nayatolea Macho tu mpaka njaa inaniuma!!!
Mdau Peter Mugisha Piere(Obama)Nkurunziza akiwajibika.
Kushono ni kijana Evody(chinga)akipata Mulo pamoja na kaka zake.
Bibi huyu mlemavu wa miguu akitwanga Menu kwa raha zake.
Wa dada hawa pamoja na majukumu ya hapa na pale ya kila siku,ufika wakati uwa wanamkumbuka mungu kwa sala na toba,sadaka na kwenda kwenye nyumba za ibada,hapa nao wakipata msosi.
Mdau huyu alitambulika kama Balozi,hapo akitoa neno la kushukuru ujio na msosi kwa ujumla.
Ulifika wakati wa kutoa zawadi binafsi,juice,sabuni,nguo etc
Mkurugenzi MugishaPiere alikuwa busy muda flani kurekodi matukio muhimu,huyu ni mlezi wa BUKOBAWADAU BLOG.
Mrs Hope Makoko akichapa story kwa upendo mkuu na bibi huyu Mcheshi.
Hatimaye Nyota ikamuwakia Balozi,akasema hapa sitoki kapa aaah aaah kuopoa hakuna Umri,dada Chui kadai watu wazima wanajua kubembeleza,kutunza na kusamehe,kosea uruke na tu Janki kama....kila siku bifuuuuu !!!
Wadau katika picha ya pamoja na Wazee hawa.
Baada ya picha ya pamoja kilichofata ni kuwarudisha wazee hao vyumbani,mengine kuwashika mikono na wengine kuwabeba kabisa