YANAYO ONGELEWA BAADA YA KIFO CHA KANUMBA NI MENGI NA HII NI MITAZAMO YA BAADH YA WADAU
1.HUU NI MTAZAMO TU WA MDAU MMOJA KATIKA BBM GROUP.
1.Lulu alikua anaongea na nan kwenye simu?
2.kanumba alipohojiwa na MKASI alisema hanywi pombe
3.kanumba alidondoka saa 6 usiku, kapelekwa hospital saa 11 alfajiri? Hapo katikati kulitokea nin? 4.kwanin mdogo wake kanumba hakupiga simu polisi?
5.kwanin mdogo wake kanumba hakutoa huduma ya kwa kanumba?,hapa namanisha muda alioutumia kwenda kumchukua daktar kwanin asingempeleka kaka yake apatiwe first Aid pale Sinza palestina kuna dispensary ina operate 24/7?
6.ray alikua wa kwanza kufika alichukua Iniative gan?
7.kanumba alikua mtupu alipodondoka muda wakumvalisha nguo waliupata wap? Je muda huo c wangempeleka hospitali?
8.aliyefunga mlango ni lulu au kanumba?
9.kwanin mdogo wake kanumba hajashikiliwa na polisi? Kwenye nyumba walikua watu 3 first suspect ni lulu na 2nd mdogo wake kanumba,kwanin nae asikamatwe?
10.kwanin waandish wa habar,na watu wengine waliruhusiwa kuingia ktk eneo la tukio? Je ushahid si umeshapotea?
11.nyumba ya kanumba ni CRIME SCENE kwanin isingewekewa Ulinzi? Matanga yangepelekwa kwa dada ake,jeshi la polis halion limetibua ushahidi?
2. KUTOKA KATIKA UKURASA WA FACEBOOK WA WADAU,MDAU KATIKIRO MOSHI MUJAYA YEYE AMEFUNGIKA HIVI;
Mimi Binafsi nilimheshimu sana Kanumba maana alinifanya niaangalie Bongo Muvie. Watu wa karibu yangu watakuwa mashahidi. Nilistushwa sana na kifo chake, na nilikuwa kama nimepigwa ganzi hivi.
Am a thinker Maniac sikuacha kuwa huru kufikiria kifo chake hata kama ni mapenzi ya Mungu, lakini bado tuko huru na uhuru huo ni Mungu mwenyewe katupa.
...
Kuna swala la Lulu. Maskini yule mtoto katengwa, yule mtoto amechukiwa, yule mtoto anakandamizwa kisaikolojia, yule mtoto anaonwa ni Malaya, lakini kikuwa anaonwa ni muuaji kwasababu "kamuua Bongo Star Muvie" kwasababu gani "Kamuua kipenzi cha watanzania"
Nilijaribu kuvaa viatu vya Lulu, kwa kweli tunakaonea kale katoto. Tunakanyanyasa, maana siyo kweli kuwa alitoka kwao eti kuja kumuua Kanumba. Anaumizwa sana kama atakuwa anayasikia maneno ya wasanii wenzake wanavyomchukulia wakati kiukweli ni yeye na Kanumba wanajua nini kimetokea bahati mbaya sana ni yeye mwenyewe.
Nchi nzima ime-turn against Lulu.
Na wengine wamefika mbali kudhani kuwa Kanumba sasa ni Mungu mtu tusiongelee habari zake maana ni kipenzi cha watu WEH.. !

3.KATIKA UKURASA WA MDAU MUBELWA BANDIO AMEANDIKA HIVI;
IMEKWISHA.......
Sasa tuanze kujadili ya walio hai ama waliokaribia kufa.
KAMA AJALI YA NDEGE YA A.T.C huko Kigoma.
Si mmeona picha eeeee? Kwanza pale ilipo unaweza kujiuliza "hii ndege inafanya nini huku shambani?"
Japo si chanzo, lakini mwaonaje hali ya viwanja vya ndege nchini?

4.UJUMBE KUTOKA KWA MKONGWE MJENGWA
Ndugu zangu,
Ni kazi ngumu kuwa wakili kwa anayeonekana na jamii kuwa ni ‘ shetani’. Lakini, kwenye hili la kifo cha kusikitisha cha msanii Steven Kanumba kuna haja ya kukaa chini na kutafakari kwa bidii.
Kuna maswali pia ya kujiuliza juu ya msichana huyu wa miaka 18 ambaye sehemu kubwa ya jamii imeshamuhukumu kuwa ni muuaji.
Kuna hata ambao hawalijui jina lake la kamili, bali, anajulikana kama ‘ Lulu’. Jina lake ni Elizabeth Michael .
Simulizi ya Lulu inaonyesha kuwa yeye na Kanumba walikuwa na mahusiano. Na wivu pia umeingia kwenye mahusiano yao. Hivyo basi, ugomvi na hatimaye kifo cha Kanumba.
Uchunguzi kamili haujakamilika. Na kama haujakamilika, basi, Lulu anabaki kuwa ni mtuhumiwa na si muhusika na kifo hicho. Kumwita Lulu muuaji ni kuharakisha kutoa hukumu isiyo ya haki. Pamoja na machungu yetu, lakini wanadamu tunapaswa kuwa na subira.
Na ukweli unabaki, kuwa Lulu ni mwanadamu kama wewe na mimi. Na kwa yote yaliyotokea, anabaki kuwa ameondokewa na mpenzi wake. Je, ni nani anaye
mfariji msichana huyu wa miaka 18 aliyeondokewa na mpenzi wake?
Maggid Mjengwa,
Dar es Salaam.
0788 111 765
Dar es Salaam.
0788 111 765